Vifungo vya kisiasa kama matokeo ya kuporomoka kwa demokrasia
Matokeo Makuu ya Utafiti
Vifungo vya kisiasa ni nyenzo muhimu ya kupunguza upinzani, na huambatana na mmomonyoko mkubwa wa kidemokrasia. Hukumu, vizuizi na vifungo vya kisiasa, na mashtaka dhidi ya wapinzani wa serikali yaliongezeka wakati wa mvutano wa kisiasa katika nchi sita zilizoshuhudia kudorora kwa demokrasia hivi karibuni: Nikaragua, Tanzania, Thailand, Tunisia, Uturuki, na Venezuela. Walengwa wamekuwa wakishikiliwa kizuizini kwa muda mrefu bila hukumu rasmi ya mahakama, kuzuiwa ushiriki wao kufanya siasa za upinzani, uandishi wa habari, na katika shughuli za utetezi wa haki za binadamu. Pamoja na athari za kimwili, vifungo hivi husababisha athari za kisaikolojia na gharama kubwa ya kifedha kwa wafungwa ambazo pia huweza kuwaathiri familia za wafungwa.
Kwa kila mfungwa wa kisiasa aliye mahabusu, wapinzani wengi zaidi wa serikali wanakabiliwa na vikwazo vya hila vinavyopelekea "kifo cha uraia". Viongozi wanaopinga demokrasia wamelenga wapinzani na wakosoaji wa serikali kwa kutumia aina zingine za ukandamizaji ambazo zinazuia wapinzani kufanya kazi zao na kuminya ushiriki wao katika jamii – hali ambayo wataalam wanaita “kifo cha uraia”. Mbinu zinazotumiwa na serikali zisizo za kidemokrasia kufanikisha kifo cha uraia ni pamoja na udhibiti wa safari, kufuatilia kwa ukaribu nyendo za walengwa, kuorodhesha walengwa kwenye orodha ya watu hatari, na kukamata mali zao. Vizuizi hivi kwa kawaida hutokea kwa mjumuiko, na vinaweza kutekelezwa kwa njia rasmi na zisizo rasmi, na watendaji wa serikali na wasio wa serikali. Tulishuhudia kwa ujumla wake vizuizi hivi vinavyopelekea kifo cha uraia katika kila moja ya nchi sita zilizofanyiwa utafiti.
Mahakama zisizo huru huwezesha vifungo vya kisiasa na kifo cha uraia kwa amri na matakwa ya tawala za kiimla. Viongozi wenye uwezo wa kudhibiti mhimili wa mahakama huweza kuzitumia korti kama nyenzo kubwa ya ukandamizaji. Walengwa wa ukandamizaji huo hupoteza ufikiaji wa njia muhimu za rufaa na uwajibikaji kipindi ambacho mahakama inatenda kwa masilahi ya serikali. Watendaji wa Mahakama wenye fikra na misimamo huru wapo katika hatari ya kuwa walengwa wa ukandamizaji wa serikali, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwenye nafasi zao na kisha nafasi zao kupewa wafuasi waaminifu kwa serikali, hali inayopelekea kumomonyoka zaidi kwa mhimili wa mahakama.
Kupinga vifungo vya kisiasa na kifo cha uraia ni muhimu katika kupigania uhuru. Vifungo vya kisiasa na kifo cha uraia huwezesha viongozi wasioheshimu utawala wa kidemokrasia kuwaondoa wakosoaji wao wenye nguvu na ufanisi kutoka kwenye jamii. Mbinu hizi zinaweza kutokea katika nchi zinazokabiliwa na wimbi la mmomonyoko wa demokrasia, lakini hazijafikia kuwa tawala za kimabavu. Ufuatiliaji wa mwenendo wa mbinu za vifungo vya kisiasa na kifo cha uraia, na kuchukua hatua stahiki kwa wakati husika ni muhimu katika mapambano dhidi ya utawala wa kimabavu, kusaidia mawakala wa mabadiliko ya kidemokrasia, na kuzuia mawimbi ya ukandamizaji katika siku zijazo.
Utangulizi
Dola haiishiwi mbinu katika kujaribu kuwatisha watu ili wakae kimya.1 – Nukuu kutoka kwa Mwanaharakati wa asasi za kiraia nchini Tanzania.
Kiongozi wa upinzani yupo mahabusu, akishutumiwa kwa uhalifu danganyifu kuelekea uchaguzi mkuu wa taifa. Kijana wa kike ameshtakiwa kwa kukashifu utawala wa kiimla baada ya kudai mabadiliko ya kidemokrasia katika taifa lake. Kijana huyo amezuiliwa kurejea masomoni hata baada ya kuachiliwa huru kutoka kizuizini kwa dhamana. Mtetezi wa haki za binadamu anapojaribu kusafiri nje ya nchi kikazi anagundua kuwa anachunguzwa kwa makosa ya ugaidi na amewekwa chini ya marufuku ya kusafiri. Huku mwenzake akiwekwa kizuizini kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya hukumu. Jaji anafukuzwa kazi baada ya rais wa nchi yake kusimamisha bunge; kisha mafao yake ya kazi na bima ya afya yakazuiliwa.
Hii ni mifano michache tu ya jinsi tawala zisizo za kidemokrasia zinavyozuia wapinzani wa kweli na wanaodhaniwa - wakiwemo watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wanaharakati wa kisiasa, viongozi wa upinzani, watumishi wa umma, waasi wa serikali, waandamanaji, na raia wa kawaida – kuweza kuongoza maisha yao. Mbinu inayoonekana zaidi ni vifungo vya kisiasa, iwe kwa kupitia mashtaka yaliyotengenezwa kisiasa na hukumu zake, au hatua za kabla ya kesi zinazoweza kuwaweka watu kizuizini kwa miezi au miaka kabla ya kesi zao kutatuliwa.
Lakini kwa kila mfungwa wa kisiasa aliye mahabusu, wapinzani wengi wa serikali na wakosoaji wanakabiliwa na vikwazo vya hila, vinavyolingana na kile baadhi ya wataalam wanachokiita "kifo cha uraia." Ingawa neno hilo lina maana tofauti katika nyanja tofauti za kitaaluma2, Freedom House inachukulia dhana ya kifo cha uraia kama hali ambayo wapinzani wa serikali wanazuiliwa kushiriki katika jamii kupitia mjumuiko wa njia mbalimbali za ukandamizaji, ikiwemo udhibiti wa safari, ufuatiliaji wa karibu wa nyendo za walengwa, kuorodhesha walengwa kwenye orodha ya watu hatari, na kukamata mali zao. Kwa vitendo, mbinu hizi hujidhihirisha kupitia marufuku ya kusafiri na kunyang’anywa hati za kusafiria, vyombo vya ulinzi hasa polisi kuweka kambi nje ya nyumba ya mlengwa ili majirani wote waone, ugumu wa kupata au kuendelea na kazi kwa sababu ya unyanyapaa wa kijamii au kuorodheshwa kwenye orodha ya watu hatari, kufukuzwa chuo, kunyang’anywa mali, na kufungwa kwa akaunti za benki. Mbinu hizi zinaweza kuunganishwa na masharti ya kuachiliwa kutoka kizuizini au kifungo cha kisiasa, au kutolewa kwa njia yake pekee, iwe kwa amri rasmi au kupitia shinikizo la kijamii. Mara nyingi, walengwa wanakabiliana na zaidi ya njia moja kwa wakati mmoja, na athari zinazoongezeka huwazuia kufanya kazi au kuishi maisha ya kawaida.
Vifungo vya kisiasa3 na, kwa kiwango fulani, mbinu za ukandamizaji zinazosababisha kifo cha uraia, vimeshamiri kwa kiasi kikubwa katika nchi zenye historia ndefu ya utawala wa kimabavu, kama vile China, Iran, na Korea Kaskazini. Lakini, matumizi ya mbinu hizi kwa lengo la kuadhibu na kunyamazisha wapinzani na wakosoaji yamekuwa dhahiri pia katika maeneo ambayo yamekumbwa na mmomonyoko wa kidemokrasia hivi karibuni. Kupitia utafiti wetu, tumejikita kutathmini na kuelewa mwenendo wa viongozi wanaotamani utawala wa kiimla au viongozi waliopo madarakani katika serikali za kiimla wanavyokandamiza wapinzani, na jinsi mbinu hizo zinavyodhihirika katika nyakati za uharibifu wa kidemokrasia. Ripoti hii inachunguza mienendo kama hii katika nchi sita zilizopitia kushuka kwa demokrasia kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka 20 iliyopita: Nikaragua, Tanzania, Thailand, Tunisia, Uturuki, na Venezuela.
- 1Interview with a Tanzanian civil society actor who requested anonymity, July 2023.
- 2The term “civil death” has been used in various ways in other fields of study, including in analysis of antiquated and contemporary law, and to characterize discrimination against people with disabilities or who face certain diseases, among others. Gabriel J. Chin, “The New Civil Death: Rethinking Punishment in the Era of Mass Conviction,” University of Pennsylvania Law Review 160, no. 6 (2012): 1789-1833, https://scholarship.law.upenn.edu/cgi/viewcontent.cgi?article=1067&cont…; National Council on Disability, “Beyond Guardianship: Toward Alternatives That Promote Greater Self-Determination,” March 22, 2018, https://ncd.gov/sites/default/files/NCD_Guardianship_Report_Accessible…; Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights, “UN rights expert urges action to end ‘civil death’ of persons affected by leprosy,” June 19, 2018, https://www.ohchr.org/en/press-releases/2018/06/un-rights-expert-urges-….
- 3“Political imprisonment” is used in this report as a shorthand for politicized prison sentences, as well as politicized detentions, prosecutions, and investigations against real or perceived government opponents or critics. “Government opponent” includes critics and those voicing dissent.
Ripoti hii imetokana na mahojiano na wataalam 42 wa nchi, yakiongezewa na utafiti wa mezani. Miongoni mwa waliohojiwa ni watendaji wa mashirika ya kiraia, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, watafiti, na wanazuoni; baadhi yao wamevumilia vifungo vya kisiasa na chembechembe za kifo cha uraia. Nukuu zimehaririwa ili kueleweka kwa urahisi.
Vifungo vya kisiasa vimechangia kupunguza upinzani katika mazingira mapana ya mmomonyoko wa kidemokrasia katika kila moja ya nchi sita zilizofanyiwa utafiti. Zaidi ya hayo, tulibaini mbinu zinazochangia kifo cha uraia - udhibiti wa safari, ufuatiliaji wa karibu wa nyendo za walengwa, kuorodhesha walengwa kwenye orodha ya watu hatari, na kukamata mali zao – zimetokea pia katika nchi zote sita. Vifungo vya kisiasa na hatua za kifo cha uraia zimetokana na upokaji wa madaraka kwa njia zisizo za kidemokrasia, maandamano makubwa ya kupinga serikali, na kampeni za uchaguzi. Kwa kuongezea, vifungo vya kisiasa na hatua za kifo cha uraia hutumiwa katika nchi ambazo bado hazijafikia kuwa tawala kamili za kimabavu; matumizi yao hayakuanza kabla ya kufikia kina cha utawala wa mabavu (na wengine bado hawajafikia) bali katika maeneo ambayo kila nchi ilikadiriwa Huru kwa kiasi au Huru kwa mujibu wa Freedom in the World, ripoti ya mwaka ya Freedom House juu ya haki za kisiasa na uhuru wa raia. Tumebaini kwamba vifungo vya kisiasa na kifo cha uraia hutokea sambamba na uharibifu wa demokrasia.
Hatari ya mbinu hizi ni kwamba zitatumiwa dhidi ya watetezi wa kidemokrasia wenye msimamo mkali, wanaofanya kazi kwa ujasiri katika nchi zote ulimwenguni zinazokabiliwa na mmomonyoko wa kidemokrasia. Mbali na kufanikiwa kuwaondoa wapinzani na wakosoaji kwenye jamii, vifungo vya kisiasa na kifo cha uraia vinaweza kuwa na madhara makubwa ya kimwili, kisaikolojia, na kiuchumi kwa walengwa wa ukandamizaji huu, pamoja na wapendwa wao. Hata hivyo, bado fursa za kupata msaada wa kisheria na uwajibikaji zipo chache, kwani mifumo ya mahakama legelege husaidia kufungwa pasipo kufata haki, na majaji wenyewe wanaweza kuwa walengwa wa ukandamizaji endapo hawatii utaratibu huu.
“Wanatumia aina yoyote ya nyenzo wanayoweza kutumia ili kudhibiti jamii” anasema Christopher Hernandez-Roy, naibu mkurugenzi na mshiriki mwandamizi wa Programu ya Amerika katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa, ambaye ametafiti na kuandika kuhusu vitendo vikali vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika kipindi cha ukandamizaji mkubwa nchini Venezuela1. Hata hivyo, bado kuna shinikizo kubwa kutoka kwa makundi mbalimbali kupinga utawala wa kimabavu.
- 1Interview with Christopher Hernandez-Roy, Senior Fellow and Deputy Director, Americas Program, Center for Strategic and International Studies, August 2023.
Vifungo Vinavyoonekana: Vifungo vya kisiasa kama matokeo ya kuporomoka kwa demokrasia
Waliwakamata wanasiasa maarufu, viongozi wa vyama vya siasa, hakimu na mawakili. Mimi ni nani? Naweza kutoweka, na hakuna mtu atakayesikia habari zangu1 – Mtendaji wa asasi za kiraia
Hukumu za kisiasa, vizuizi, na mashtaka hutokea duniani kote, lakini matumizi yake hayakomei pekee kwa tawala ngumu zaidi za kimabavu. Mbinu hizi zimepatikana katika maeneo yenye aina nyingi za mmomonyoko wa kidemokrasia, kama inavyoonyeshwa katika kila moja ya mifano sita iliyochunguzwa na Freedom House kwenye utafiti huu. Tulibaini kuwa vifungo vya gerezani huibuka kama matokeo ya kuvunjika kwa taasisi za kidemokrasia, kwa ghafla ama kwa taratibu, pamoja na athari kubwa za kimwili, kisaikolojia, na kifedha kwa wafungwa na watu wao wa karibu.
Kushamiri kwa vifungo wa Kisiasa
Upokaji wa madaraka, ikiwemo kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi, mara nyingi hujumuisha kampeni kali za vifungo vya kisiasa ambazo huongeza ugumu na gharama za kupinga vitendo visivyo vya kidemokrasia. Mamia ya watu wakiwemo wanasiasa, waandishi wa habari, na wanaharakati, waliwekwa kwenye vizuizi vya kijeshi baada ya mapinduzi ya mwaka 2014 nchini Thailand2, taifa ambalo limekuwa likiandamwa na mapinduzi ya kijeshi. Wengi wa wahanga hawa, walishikiliwa kwa muda wa hadi siku saba, mbinu iliyojulikana kama "marekebisho ya mtazamo."3 Kufuatia maendeleo makubwa ya kidemokrasia nchini Tunisia katika kipindi cha miaka kumi baada ya kuondolewa madarakani kwa Zine el-Abidine Ben Ali mwezi Julai 2021, Rais Kaïs Saïed alisimamisha bunge, na hatimaye kulivunja mwaka uliofuata, pamoja na kuvunja na kuzifuta taasisi mpya za kidemokrasia, kisha kuendesha kura ya maoni ya katiba iliyoimarisha madaraka ya mhimili wa Serikali. Tangu Saïed achukue madaraka, angalau viongozi nane wa vyama vikubwa vya upinzani waliwekwa kizuizini kabla ya hukumu kwa mashtaka yasiyothibitishwa juu ya usalama wa taifa, pia waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu wamekamatwa chini ya sheria mpya kandamizi ya uhalifu wa mtandao, na wafanyabiashara, mawakili, na wengineo wamejikuta wakihusishwa kwenye kesi zisizojulikana za “kula njama dhidi ya serikali”4.
Mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa nchini Uturuki yamechochea kumomonyoka kwa demokrasia pamoja na vifungo vya kisiasa. Baada ya jaribio la mapinduzi la mwaka 2016, Rais Recep Tayyip Erdoğan alishinikiza mageuzi ya katiba ambayo kimsingi yaligeuza Uturuki kuwa nchi inayotawaliwa kwa amri ya Rais. Madaraka hayo mapya yamempa Rais Erdoğan nguvu ya kumfunga gerezani na kumuweka kizuizini mtu yeyote anayeonekana kuwa tishio kwa utawala wake: mtendaji wa asasi ya kiraia nchini Uturuki alinukuliwa akisema kuwa "Yeyote mwenye mtazamo tofauti anafuatiliwa,”5. Waandishi wa habari, wafuasi wa vyama wa upinzani, na wanazuoni ni miongoni mwa wale ambao wamekabiliwa na madhila ya kuwekwa kizuizini bila hukumu rasmi kwa mda mrefu au hukumu kali gerezani6.
Tawala zilizodumu kwa muda mrefu madarakani ambazo bado hazijakita mizizi kikamilifu kwenye mifumo ya kimabavu, hutumia pia mbinu hii ya kuwafunga wapinzani wake kisiasa, huku viwango vya kuweka kizuizini vikibadilika kutofautiana na wakati. Nchini Tanzania, mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli alitangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliotawaliwa na ushindani mkali isiyo kawaida mwaka 2015. Utawala wake ulianzisha ukandamizaji uliowalenga wanasiasa wa upinzani, vyombo vya habari, asasi za kiraia; na kila aliyeonekana kikwazo kwa watawala. Sheria kandamizi mpya na zilizokuwepo awali zilitumika kuwalenga wapinzani, ikiwemo sheria ya kusimamia na kudhibiti vyama vya siasa na marufuku ya mikutano ya kisiasa iliyotumika makusudi kwa wapinzani na kusabisha watu kukamatwa7.
Upinzani dhidi ya kushamiri kwa tawala za kimabavu kwenye nchi za Nikaragua na Venezuela ulisababisha ukandamizaji wa kutisha, ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kuwaweka kizuizini watu wengi kiholela pasipo kuzingatia taratibu na haki. Matumizi haya ya mabavu yaliwezekana mara baada ya kuvunjwa kwa utaratibu wa taasisi za kidemokrasia na uimarishaji wa mamlaka ya Rais. Rais Hugo Chávez wa Venezuela alitengeneza mazingira wezeshi ya kisiasa na kisheria ya kumfunga kisiasa mrithi wake Nicolás Maduro, kwa kuingilia mahakama sambamba na matumizi ya sheria mbalimbali kandamizi. Ingawa Chávez hakuwa na utamaduni wa kuwakamata na kuwafunga wapinzani wake mara kwa mara8, Maduro alionekena kupendelea zaidi mbinu hiyo ya kufunga kisiasa na kutumia mabavu kupita kiasi, hasa nyakati za maandamano ya kisiasa makubwa ya kupinga serikali mwaka 2014, 2017, na 20199. “Kupitia utawala wa Maduro, tulichokiona ni kurudi kwa ukandamizaji wa kimfumo - kukamatwa kiholela, unyanyasaji mitaani, kutofuatwa kwa utaratibu wa kisheria, na mateso makali kizuizini," Tamara Taraciuk Broner, mkurugenzi wa Programu ya Utawala wa Sheria kwa ajili ya Mjadala wa Inter-American, aliiambia Freedom House10. Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Foro Penal, karibu watu 16,000 walifungwa kisiasa nchini Venezuela kati ya Januari 2014 na Desemba 2022. Kwa mujibu wa shirika hilo, hadi Rais Chavez anafariki dunia mwaka 2013 kulikuwa na wafungwa wa kisiasa takriban 11 nchini humo11.
- 1Interview with Radwan Masmoudi, president of the Center for the Study of Islam and Democracy, August 2023, speaking on behalf of citizens and activists based in Tunisia.
- 2Jonathan M. Powell and Clayton L. Thyne, “Global Instances of Coups from 1950 to 2010: A New Dataset,” Journal of Peace Research 48, no. 2 (2011): 249-259, https://www.uky.edu/~clthyn2/coup_data/home.htm.
- 3Human Rights Watch, “To Speak Out is Dangerous: Criminalization of Peaceful Expression in Thailand,” October 24, 2019, https://www.hrw.org/report/2019/10/25/speak-out-dangerous/criminalizati…. See also interviews with Akarachai Chaimaneekarakate, advocacy lead for Thai Lawyers for Human Rights, August 2023; Tyrell Haberkorn, Director of Graduate Studies, Professor of Southeast Asian Studies, University of Wisconsin-Madison, July 2023; and Bencharat Sae Chua, Institute of Human Rights and Peace Studies, Mahidol University, Thailand, July 2023.
- 4Amnesty International, “Human rights under assault two years after President Saied’s power grab,” July 24, 2023, https://www.amnesty.org/en/latest/campaigns/2023/07/human-rights-under-….
- 5Interview with a Turkish civil society actor, June 2023.
- 6Human Rights Watch, “Turkey: Government Targeting Academics,” May 14, 2018, https://www.hrw.org/news/2018/05/14/turkey-government-targeting-academi…; Human Rights Watch, “Turkey: Release Politicians Wrongfully Detained for 7 Years,” November 3, 2023, https://www.hrw.org/news/2023/11/03/turkey-release-politicians-wrongful…; Media and Law Studies Association (MLSA) Stakeholder report, Universal Periodic Review 35th Session, Turkey.
- 7American Bar Association, Center for Human Rights, “Submission by the American Bar Association, Center for Human Rights (ABA CHR) in respect of the third periodic cycle of the Universal Periodic Review (UPR) of the United Republic of Tanzania, 39th Session of the UPR Working Group (October - November 2021),” June 2021, https://www.americanbar.org/content/dam/aba/administrative/human_rights…; Freedom House, “Tanzania,” in Freedom in the World 2019, https://freedomhouse.org/country/tanzania/freedom-world/2019.
- 8See, for example, interviews with Christopher Hernandez-Roy, Senior Fellow and Deputy Director, Americas Program, Center for Strategic and International Studies, August 2023; and Tamara Taraciuk Broner, Rule of Law Program Director for Inter-American Dialogue, August 2023.
- 9Interview with a representative from the Center for Defenders and Justice, July 2023.
- 10Interview with Tamara Taraciuk Broner, Rule of Law Program Director for Inter-American Dialogue, August 2023.
- 11Foro Penal, “Reporte sobre la represión en Venezuela. Año 2022 [Report on repression in Venezuela in 2022],” February 12, 2023, https://foropenal.com/reporte-sobre-la-represion-en-venezuela-ano-2022/; Alfredo Romero, “The Repression Clock: A Strategy Behind Autocratic Regimes,” Wilson Center Latin American Program, July 2020, https://www.wilsoncenter.org/sites/default/files/media/uploads/document….
Mmomonyoko wa demokrasia nchini Nikaragua ulichagizwa kwa kasi baada ya Daniel Ortega kuchaguliwa kuwa Rais nchini humo mwaka 2006. Ortega, ambaye amekuwa akijilimbikizia madaraka, alisimamia ukandamizaji mkali, hasa baada ya pendekezo la serikali yake la kupunguza pensheni iliyopelekea maandamano makubwa ya kupinga pendekezo hilo mwezi Aprili 2018; hadi katikati ya mwaka huo zaidi ya watu 1,900 walikamatwa, wakiwemo viongozi wa upinzani, wanaharakati, wanazuoni na waandishi wa habari1. Ukamataji uliendelea, na kuongezeka kwa mara nyingine tena kuelekea uchaguzi uliogubikwa na udanganyifu mwaka 20212. Katika ripoti yake ya Machi 2023, Kundi la Wataalamu wa Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu Nikaragua lilisema lina sababu za kutosha kuamini kuwa ukiukwaji na unyanyasaji uliofanyika tangu mwaka 2018, ulioamriwa na utawala wa Ortega, ulilingana sawa na uhalifu dhidi ya ubinadamu3.
Viongozi wengi wameongeza matumizi ya vifungo vya kisiasa kukabiliana na changamoto za kisiasa ikiwemo maandamano ya amani, na kupunguza kasi ya upinzani. Maandamano makubwa ya vijana ya kudai demokrasia nchini Thailand mwaka 2020 na 2021 yaliyojitokeza kwa kiasi fulani kupinga uamuzi wa mahakama wa kufuta chama kikuu cha upinzani4, yalikabiliwa na kukamatwa kwa waandamanaji: hadi Agosti 2023, takriban watu 2,000 waliripotiwa kushtakiwa kwa makosa ya jinai yanayohusiana na maandamano hayo5. Nchini Uturuki, polisi walizuia kwa mabavu maandamano ya Gezi Park ya mwaka 2013, ambayo yalianza kama pingamizi la kubomolewa kwa eneo la mapumziko, lakini yakabadilika kuwa maandamano ya kitaifa dhidi ya serikali6. Wakati maelfu ya watu walikamatwa – kile kilichojulikana kama "Mashtaka ya Gezi" yalifikia kilele chake mwaka 2022 ambapo wanaharakati nane walihukumiwa kwa madai ya njama; kati yao, watano walibaki gerezani hadi Novemba 2023.7
Kufungwa kwa wanaharakati, wapinzani, waandishi wa habari, na makundi mengine yanayopinga unyanyasaji wa serikali, kuna athari kubwa kwa afya na ustawi wa demokrasia ya nchi husika. Kuondolewa kwa makundi haya katika jamii kunaruhusu viongozi wa kimabavu na wenye mwelekeo huo kutekeleza unyanyasaji bila upinzani mkubwa, na wale wanaosalia huru wana uwezekano mdogo wa kuhoji na kutoa maoni yao kwa kuhofia kukamatwa na kufungwa hapo baadae. "Wakati mwingine pia nadhani serikali inapenda (wafungwa wa kisiasa wa zamani wa Venezuela) wasimulie hadithi zao, kwa sababu hilo pia linaongeza hofu kwa wengine,” Franz von Bergen, mwandishi wa habari wa Venezuela, aliiambia Freedom House.8
- 1Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights, “Human Rights Violations and Abuses in the Context of Protests in Nicaragua 18 April - 18 August 2018,” August 2018, https://www.ohchr.org/sites/default/files/Documents/Countries/NI/HumanR….
- 2“OAS members condemn Nicaragua elections, urge action,” Reuters, November 12, 2021, https://www.reuters.com/world/americas/oas-members-condemn-nicaragua-el…; UN Human Rights Council, Report of the Group of Human Rights Experts on Nicaragua, A/HRC/52/63 (March 2, 2023). See also interviews with Yaritzha Mairena, representative of the National Union of Nicaraguan Political Prisoners, August 2023; Lucas Perelló, assistant professor of political science, Marist College, June 2023; a Nicaraguan human rights lawyer who requested anonymity, August 2023; a Nicaraguan journalist, July 2023; and a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
- 3UN Human Rights Council, Report of the Group of Human Rights Experts on Nicaragua, A/HRC/52/63 (March 2, 2023).
- 4Rebecca Ratcliffe, “Thai court dissolves opposition party Future Forward,” Guardian, February 21, 2020, https://www.theguardian.com/world/2020/feb/21/thai-court-dissolves-oppo….
- 5Interview with Akarachai Chaimaneekarakate, advocacy lead for Thai Lawyers for Human Rights, August 2023.
- 6Amnesty International, “Gezi Park protests: Brutal denial of the right to peaceful assembly in Turkey,” October 2, 2013, https://www.amnesty.org/en/documents/EUR44/022/2013/en/.
- 7Human Rights Watch, “Turkey: Top Court Upholds Rights Defender’s Life Term,” October 10, 2023, https://www.hrw.org/news/2023/10/10/turkey-top-court-upholds-rights-def….
- 8Interview with Franz von Bergen, Venezuelan journalist, June 2023.
Vitisho kwa familia na wapendwa
Mbali na uharibifu endelevu wanaopata asasi za kiraia kipindi wakosoaji na wapinzani wa serikali wanapofungwa gerezani, madhara yanayosababishwa na vifungo vya kisiasa kwa wahanga na familia zao ni makubwa na ya kudumu kwa mda mrefu. Katika tafiti zetu kwenye nchi sita, wataalam wamebainisha kwamba wafungwa wa kisiasa hupata madhara makubwa ya kimwili na kisaikolojia. Matumizi mabaya yalihusisha mateso ya kimfumo ulioratibiwa na vyombo vya dola nchini Nikaragua na Venezuela, pamoja na kufanyiwa ukatili wakati wa ukamataji au kizuizini, na kunyimwa haki ya kupata huduma ya matibabu.1
Sambamba na athari wanazopata wahanga wa vifungo vya kisiasa, athari husika huenda mbali hadi kuwafikia makundi mbalimbali kwenye jamii. Familia na wapendwa wao hubeba madhila na mzigo mkubwa na wanaweza kushinikizwa na mamlaka katika juhudi za kuwashawishi walengwa kuacha harakati zao au kujisalimisha, au kuendeleza mateso zaidi kwa walengwa. Wanafamilia wenyewe wamekuwa walengwa wa vizuizi vya kisiasa na mashtaka ya jinai, wakati mwingine kushambuliwa ama kupewa vitisho kutoka kwa vyombo vya dola na visivyo vya dola, ikiwemo wafuasi wa serikali na wanamgambo wasio na uhusiano na serikali.2 Nyakati zingine, matukio haya huchangia kuleta migogoro na mivutano ndani ya familia.3 Baadhi ya Ndugu wamelazimika kukimbia nchi ili wawe salama dhidi ya ukandamizaji wa mamlaka, hali inayopelekea kutengana na familia zao.4 Madhara ya kisaikolojia ya vifungo vya kisiasa, kwa wanafamilia ni makubwa na yanaweza kutokea katika vyanzo vingi, ikiwa ni pamoja na kushuhudia uvamizi na kukamatwa, kutokuwa na uhakika juu ya mahala wapendwa wao walipo, na mazingira ya kutisha wanapowatembelea wapendwa wao gerezani, kwenye mazingira yanayoruhusu ziara za gerezani.5
Matatizo ya kiuchumi wanayopitia wafungwa na familia zao pia yaliripotiwa kwenye nchi sita zilizofanyiwa utafiti huu: kwa kiasi kikubwa mlezi na anayesaidia familia ndiye huwekwa gerezani6. Upatikanaji wa dhamana na msaada wa kisheria kwa wafungwa wa kisiasa huwa ni gharama kubwa7, aidha, mahitaji ya muhimu kama chakula na dawa huhitajika kwa wafungwa, gharama ambazo ni mzigo mkubwa hususani kwa familia zenye vipato vya chini. Wakili wa haki za binadamu nchini Nikaragua, akizungumzia wafungwa wa kisiasa wenye kipato cha chini, anasema kwamba: “Ndugu na familia za wafungwa wa kisiasa wenye kipato cha chini wamekuwa wakihangaika kupata mahitaji, na ikiwa wamemletea chakula mfungwa wao, basi kuna uwezekano mkubwa kuwa wao hawajala siku hiyo”.8 Adha zingine wanazokutana nazo Ndugu na familia za wafungwa wa kisiasa ni pamoja na gharama za usafiri wanapowatembelea na kupeleka mahitaji muhimu kwa wapendwa wao, na kuhudhuria mashauri mahakamani.9 Zaidi ya hayo, athari hizi haziondoki mara tu mfungwa anapoachiliwa huru; zinaweza kudumu kwa mda mrefu. Hivyo programu zinazoundwa kusaidia wafungwa wa kisiasa zinahitaji usaidizi kamili ambao husaidia katika kupona kimwili, kihisia na kifedha.
- 1International Federation for Human Rights, “Tanzania: Arbitrary detention of Mr. Tito Magoti,” December 26, 2019, https://www.fidh.org/en/issues/human-rights-defenders/tanzania-arbitrar…; “African court orders Tunisia to allow legal access to political prisoners,” Middle East Eye, September 2, 2023, https://www.middleeasteye.net/news/african-court-orders-tunisia-allow-l…; UN Human Rights Council, Detailed findings of the independent international factfinding mission on the Bolivarian Republic of Venezuela, A/HRC/45/CRP.11 (September 15, 2020); UN Human Rights Council, Report of the Group of Human Rights Experts on Nicaragua, A/HRC/52/63 (March 2, 2023). See also, for example, interviews with Javier Corrales, Dwight W. Morrow 1895 professor of Political Science, Amherst College, August 2023; Nate Grubman, political scientist researching Tunisian politics, June 2023; Yaritzha Mairena, representative of the National Union of Nicaraguan Political Prisoners, August 2023; Fulgence Massawe, director of advocacy and reforms for the Legal and Human Rights Centre, July 2023; a representative from the Venezuelan Observatory of Social Conflict, August 2023; a scholar focused on Tanzania who requested anonymity, August 2023; and a scholar focused on Venezuela, August 2023.
- 2“Confirman condena de ocho y diez años de cárcel a familiares del opositor exiliado, Javier Álvarez [Relatives of exiled opposition leader sentenced to 8 and 10 years in prison],” Confidencial, January 18, 2023, https://confidencial.digital/nacion/confirman-condena-de-ocho-y-diez-an…; “Thai activist’s mother charged under royal insult laws over Facebook post,” Reuters, August 1, 2016, https://www.reuters.com/article/us-thailand-politics-idUSKCN10C230/; Alfredo Romero, “The Repression Clock: A Strategy Behind Autocratic Regimes,” Wilson Center Latin American Program, July 2020, https://www.wilsoncenter.org/sites/default/files/media/uploads/document…; UN Human Rights Council, Detailed findings of the independent international factfinding mission on the Bolivarian Republic of Venezuela, A/HRC/45/CRP.11 (September 15, 2020); José Urrejola, “Secuestros de familiares de opositores en Nicaragua [Kidnappings of relatives of opponents in Nicaragua],” Deutsche Welle (DW), September 19, 2022, https://www.dw.com/es/secuestros-de-familiares-de-opositores-en-nicarag…. See also interviews with a civil society actor focused on Thailand who requested anonymity, June 2023; Howard Eissenstat, associate professor, St. Lawrence University, July 2023; Tamara Taraciuk Broner, Rule of Law Program Director for Inter-American Dialogue, August 2023; and Jesús Tefel, Nicaraguan activist, July 2023.
- 3See, for example, interviews with Pavin Chachavalpongpun, a Thai scholar and activist, July 2023; Akarachai Chaimaneekarakate, advocacy lead for Thai Lawyers for Human Rights, August 2023; a civil society actor focused on Thailand who requested anonymity, June 2023; and an activist focused on Tunisia who requested anonymity, August 2023.
- 4See, for example, interviews with Tamara Taraciuk Broner, Rule of Law Program Director for Inter-American Dialogue, August 2023; Jesús Tefel, Nicaraguan activist, July 2023; and a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
- 5Interviews with Pavin Chachavalpongpun, a Thai scholar and activist, July 2023; Tamara Taraciuk Broner, Rule of Law Program Director for Inter-American Dialogue, August 2023; a Nicaraguan human rights defender, August 2023; and a civil society actor based in Turkey who requested anonymity, July 2023.
- 6UN Human Rights Council, Detailed findings of the independent international factfinding mission on the Bolivarian Republic of Venezuela, A/HRC/45/CRP.11 (September 15, 2020). See also interviews with Kevin Hewison, Emeritus Professor, Department of Asian Studies, The University of North Carolina at Chapel Hill, July 2023; Yaritzha Mairena, representative of the National Union of Nicaraguan Political Prisoners, August 2023; Radwan Masmoudi, president of the Center for the Study of Islam and Democracy, August 2023; Lucas Perelló, assistant professor of political science, Marist College, June 2023; Jesús Tefel, Nicaraguan activist, July 2023; a Nicaraguan journalist, July 2023; a Nicaraguan human rights defender, August 2023; a Tanzanian civil society actor, August 2023; and a civil society actor based in Turkey who requested anonymity, July 2023.
- 7See, for example, interview with Aikande Kwayu, independent political analyst in Tanzania, August 2023.
- 8Interview with a Nicaraguan human rights lawyer who requested anonymity, August 2023.
- 9See, for example, interviews with Tyrell Haberkorn, Director of Graduate Studies, Professor of Southeast Asian Studies, University of Wisconsin-Madison, July 2023; a Nicaraguan human rights lawyer who requested anonymity, August 2023; and a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
Vifungo Visivyoonekana: Athari za Kifo cha uraia
Kifo cha uraia kilikuwa kibaya sana.1 – Mtetezi wa haki za binadamu wa Nikaragua
Kuweka wapinzani na wakosoaji wa serikali kizuizini na gerezani ni mkakati unaodhihirika zaidi wa kuwaondoa watu kwenye jamii. Hata hivyo, nje ya vizuizi na magereza, kuna mfululizo wa mikakati mingine mingi inayoharibu uwezo wa watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wanaharakati wa kisiasa na viongozi wa upinzani, na wengine wengi, kuishi maisha ya kawaida, na hata kuendelea na kazi inayolenga kukuza demokrasia na haki za binadamu. Baadhi ya wahojiwa walielezea hali hii kama “kifo cha uraia.”2 Kifo cha uraia pia kimetambuliwa kama mbinu inayotumiwa na wafuasi wa viongozi wa kimabavu. Kwa mfano mwaka 2016, mwandishi wa habari anayeunga mkono serikali nchini Uturuki alitoa wito kwa wasomi wanaopinga serikali kukabiliwa na “kifo cha uraia”.3
Kifo cha uraia kama dhana, siyo mpya na imekuwa ikitumika katika muktadha tofauti tofauti katika machapisho mbalimbali. Kifo cha uraia kimetuka kumaanisha masharti wanayopitia wapinzani na wakosoaji wa serikali katika mazingira ya tawala za kimabavu, au uchambuzi wa sheria za kisasa na za zamani zilizotumia neno hilo, na ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu au magonjwa fulani.4 Kwa lengo la utafiti huu, tunazingatia zaidi tafsiri ya kwanza: kuwa ‘kifo cha uraia’ ni hali ya kuwanyima wapinzani haki ya kushiriki katika jamii kupitia njia mbalimbali za mbinu kandamizi. Ingawa sio orodha kamili, tumezigawa mbinu hizi kwa upana wake kama: kudhibiti safari za ndani na nje ya nchi, ufuatiliaji wa karibu wa nyendo za walengwa, kuzuia fursa za ajira na elimu na huduma za serikali (kuweka kwenye orodha ya watu hatari), na kushikilia mali na vitu vingine vya walengwa.
Hatua hizi zinaweza kuhusishwa na kukamatwa, kuchunguzwa, na masharti ya kuachiliwa huru, au kutumika pekee yake. Hatua hizi zinaweza kutumika rasmi, kwa taarifa au bila taarifa, au kutokana na shinikizo la kijamii. Kwa maana nyingine, kifo cha uraia ni ukumbusho wa mara kwa mara kwamba kufanya kosa moja kunaweza kusababisha kukamatwa na kuishia gerezani.
Mbinu zinazosababisha kifo cha uraia zina nguvu zaidi zinapotumiwa kwa pamoja. Kwa mfano, kumfuatilia kwa karibu mtu hupelekea kuathiri uwezo wake wa kusafiri ndani na nje ya nchi. Ufuatiliaji wa karibu wakati mwingine huonekana wazi, wakati maafisa wa vyombo vya usalama wakivamia makazi ya walengwa na kuwahoji majirani, na hivyo kusababisha shinikizo kubwa la kijamii ambalo hupelekea kuzuia fursa za kazi na kusababisha orodha isiyo rasmi ya watu hatari. Mchanganyiko wa mbinu hizi kwa ujumla wake, husisitiza kuwa kifo cha uraia si matokeo ya njia moja inayoweza kufafanuliwa kwa urahisi; badala yake, mbinu za ukandamizaji zinaingiliana na kuchanganyika ili kujenga vizuizi kutoka pande zote. Katika nchi zote sita zilizofanyiwa utafiti, tulibaini kwamba baadhi ya mjumuiko wa mbinu hizi za kifo cha uraia hutumiwa sana na mamlaka dhidi ya wapinzani na wakosoaji wa serikali.
Kwa sababu mbinu za kifo cha uraia ni za ujanja zaidi kuliko vifungo vya moja kwa moja gerezani, tawala za kikandamizaji zinaweza kuzitumia kulenga idadi kubwa ya wapinzani na wakosoaji wa serikali bila upinzani mkubwa kutoka kwa mashirika ya kimataifa, serikali za kidemokrasia, na wadau wengine wa demokrasia. Hatua hizi pia zinaweza kutumika kama nyenzo pana ya udhibiti baada ya kuisha kwa kipindi cha kifungo au kizuizi. Kwa ujumla, shinikizo linalopelekea kifo cha uraia husaidia kuzuia upinzani na ukosoaji, na hivyo kufanya iwe ngumu zaidi kutekeleza mabadiliko ya kidemokrasia kwa muda mrefu.
- 1Interview with a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
- 2See, for example, interviews with Berna Akkızal, executive director and cofounder of the Civic Spaces Association, August 2023; a Nicaraguan journalist, July 2023; a Turkish academic who requested anonymity, July 2023; and a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
- 3Cem Küçük, “‘Medeni Ölüm’ mekanizmaları! [‘Civil death’ mechanisms!],” Star, January 16, 2016, https://www.star.com.tr/yazar/medeni-olum-mekanizmalari-yazi-1082729/.
- 4See, for example, Amnesty International, “No End in Sight: Purged Public Sector Workers Denied a Future in Turkey,” May 22, 2017, https://www.amnesty.org/en/documents/eur44/6272/2017/en/; Amnesty International, “Silence at any cost: State tactics to deepen the repression in Nicaragua,” February 15, 2021, https://www.amnesty.org/en/documents/amr43/3398/2021/en/; Gabriel J. Chin, “The New Civil Death: Rethinking Punishment in the Era of Mass Conviction,” University of Pennsylvania Law Review 160, no. 6 (2012): 1789-1833, https://scholarship.law.upenn.edu/cgi/viewcontent.cgi?article=1067&cont…; National Council on Disability, “Beyond Guardianship: Toward Alternatives That Promote Greater Self-Determination,” March 22, 2018, https://ncd.gov/sites/default/files/NCD_Guardianship_Report_Accessible…; Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights, “UN rights expert urges action to end ‘civil death’ of persons affected by leprosy,” June 19, 2018, https://www.ohchr.org/en/press-releases/2018/06/un-rights-expert-urges-….
Udhibiti wa safari
Vikwazo juu ya safari za kimataifa na za ndani vilienea kwa kiasi kikubwa kwenye nchi sita zilizochunguzwa kwenye utafiti huu. Taratibu na mifumo ya kudhibiti nyendo za watu ni pamoja na marufuku ya safari, udhibiti wa pasipoti, kuhitajika kuripoti mara kwa mara kwenye vituo vya polisi au mahakamani, au hatua zingine ambazo huvuruga kwa kiasi kikubwa maisha ya kila siku na ushiriki katika jamii.
Marufuku ya kusafiri mara nyingi huambatana na uchunguzi wa jinai au hujumuishwa kama sharti la kuachiliwa huru. Nchini Nikaragua, Cristiana Chamorro, mmoja wa wagombea wa urais waliokabiliwa na uchunguzi wa jinai kabla ya uchaguzi mkuu wa 2021, aliwekwa chini ya kizuizi cha kutotoka nyumbani kwake mara baada ya kutangaza nia ya kugombea urais. Mbali na hatua zingine, Cristiana alipigwa mafuruku rasmi ya kutoondoka Nikaragua.1 Mapema mwaka 2023, nchini Tunisia, wakosoaji wawili wa serikali, Chaima Issa na Lazhar Akremi walikamatwa kwa mashtaka yasiyo na msingi ya ‘kupanga njama ya kuhatarisha na kuvuruga usalama wa taifa hilo’, na kushikiliwa kwa miezi mitano; masharti ya dhamana ya kuachiliwa kwao huru yalijumuisha marufuku ya kusafiri na ‘kuonekana kwenye maeneo ya umma’,2 ambayo ilielezewa na mwanaharakati mmoja kama "kifungo cha nyumbani kisichojidhihirisha waziwazi."3 Nchini Venezuela, baada ya mamlaka kudhibiti kimabavu maandamano makubwa ya kupinga serikali yaliyoanza mwaka 2014, wafungwa wengi wa kisiasa waliokuwa vizuzizini waliachiliwa huru chini ya masharti magumu yaliyojumuisha marufuku ya kusafiri.4
Katika baadhi ya matukio, marufuku ya kusafiri hutolewa bila wahanga kupewa taarifa. Mara tu baada ya Rais Saïed kuchukua madaraka ya kipekee mwaka 2021, serikali yake iliweka marufuku ya safari kwa raia wengi wa Tunisia, ambao wengi wao waligundua hilo mara tu walipowasili kwenye uwanja wa ndege kwa ajili ya safari. Ukosefu huu wa taarifa au nyaraka unawaacha wahanga na uwezo mdogo wa namna ya kutatua changamoto hiyo na kukata rufaa, kwa sababu mara nyingi haijulikani ni taasisi ipi ya serikali imehusika kuwawekea marufuku ya kusafiri.5
Katika hali nyingine, vikwazo tofauti vinaweza kupelekea marufuku ya kusafiri kwa vitendo. Mara baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 2014 nchini Thailand, wengi wa wanasiasa, wanaharakati, wanazuoni, na waandishi wa habari walipelekwa kwenye kambi za kijeshi kwa ajili ya kile kilichoitwa "marekebisho ya mtazamo”. Wahanga hao waliachiliwa baada ya kusaini makubaliano ya kuahidi kupata ruhusa kabla ya kusafiri nje ya nchi, kati ya masharti mengine. Kushindwa kuzingatia hilo kunaweza kusababisha kuwekwa kizuizini upya, kifungo cha gerezani, au faini.6 Vizuizi kama hivyo vya kusafiri vilijitokeza tena wakati wa maandamano ya kudai demokrasia mnamo 2020 na 2021; ambapo washtakiwa waliopewa dhamana walilazimika kupata ruhusa ya mahakama kabla ya kuondoka nchini, na mara nyingi vibali vya safari vilikataliwa.7
Ufuatiliaji wa kiusalama unaweza pia kutumika kama kizuizi cha kusafiri. Mwakilishi wa Shirika la Kupinga Mateso nchini Tunisia alielezea kwamba ziara za mara kwa mara za vyombo vya usalama hasa polisi kwenye makazi ya viongozi wa upinzani nchini Tunisia zimegeuka kuwa utamaduni wa kawaida na kuwa vizuizi vya safari za viongozi hao. “Hata kama hawajazuiliwa kusafiri, wanajikuta wakibughudhiwa na maafisa wa polisi ambao huja majumbani mwao, na kuwaelekeza kutoa taarifa kituo cha polisi kabla ya kuondoka eneo hilo”.8 Mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa 2021 nchini Nikaragua, maafisa wa polisi walianza kuwafuatilia mara kwa mara watu waliodhaniwa kuwa wagombea wa urais ambao ni Félix Maradiaga na Juan Sebastián Chamorro. Kabla ya kushtakiwa na hatimaye kuhukumiwa, vyombo vya Usalama viliwazuia viongozi hao wa upinzani kuondoka majumbani mwao na kuwajulisha kwamba wamepigwa marufuku kutoka nje ya mji mkuu wa Managua.9
Udhibiti holela wa mamlaka za serikali juu ya pasipoti, sambamba na mchakato wa uhamiaji huzuia uhuru wa kusafiri. Nchini Tanzania, uhojaji usio na msingi juu ya uraia umesababisha adha kubwa na kupelekea kunyang’anywa pasipoti kwa viongozi wa asasi za kiraia na waandishi wa habari. Uchunguzi wa namna hii unaweza kuchukua miaka mingi kukamilika, na kwa kiasi kikubwa kuzuia uwezo wa walengwa kufanya kazi na kuishi kwa uhuru.10 Tangu mwaka 2017, mamlaka za uhamiaji nchini Venezuela zimekamata au kufuta hati za kusafiria za viongozi wa upinzani, wanaharakati, waandishi wa habari, na wapinzani wengine, wakati mamlaka za serikali zikikataa kutengeneza upya au kutoa hati hizo.11 Tangu ukandamizaji wa mwaka 2018 nchini Nikaragua, imekuwa ngumu zaidi kwa watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, makasisi, maafisa wa serikali, na wafanyakazi wa mahakama kuingia au kutoka nchini, na walianza kutaifisha pasi za kusafiria mwaka 2022.12 Vivyo hivyo, kufuatia jaribio la mapinduzi la 2016 nchini Uturuki, wale wanaokabiliwa na uchunguzi walionekana ‘hawafai’ kuwa na hati za kusafiria, hata kabla ya kutolewa kwa hukumu yoyote katika mashtaka yanayowakabili.13 Hali hii ilikuja pamoja na ubatilishaji mkubwa wa hati za kusafiria za watu binafsi zaidi ya 100,000 baada ya jaribio la mapinduzi.14
Njia nyingine ya kudhibiti kusafiri na kufuatilia kwa ukaribu wapinzani na wakosoaji wa serikali ni kuwaamuru kuripoti mahakamani au kwenye kituo cha polisi mara kwa mara. Japokuwa wafungwa wa kisiasa waliohusishwa na maandamano dhidi ya serikali huko Nikaragua waliachiliwa huru kama sehemu ya makubaliano ya msamaha mwaka 2019, wengi wao bado walilazimika kujiandikisha mara kwa mara katika vituo vya polisi. Hivi karibuni, polisi wa Nikaragua walishirikiana kuwaweka kizuizini watu 57 mnamo Mei 3, 2023, waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu wakiwa miongoni mwao. Ingawa waliachiliwa huru mapema, mahakama iliwaamuru wawe wanajiandikisha kila siku kwenye kituo cha polisi kilicho karibu nao,15 jambo lililopelekea wengi kupoteza kazi zao sababu ya kulazimika kufuata sharti hilo kandamizi.16 Wafungwa wengi wa kisiasa walioachiliwa huru nchini Venezuela wanatakiwa kuripoti mahakamani mara kwa mara.17
Udhibiti wa safari unaweza kuwa na athari mbaya sio tu kwa kazi ya utetezi wa haki za binadamu, bali pia kwenye nyanja zingine kama ajira na elimu. Mwakilishi kutoka Kituo cha Watetezi na Haki cha Venezuela, akielezea hali ya mtetezi wa haki za binadamu na mwandishi habari aliyekuwa amekamatwa, alisema: “Mhanga huyu kwa kawaida hulazimika kusafiri kwenda kwenye mikutano na kutekeleza majukumu yake nje ya nchi. Moja ya adhabu walizompa ilikuwa kumzuia kusafiri nje ya nchi. Kwahiyo, kwa zaidi ya mwaka mmoja, hawezi kusafiri.”18 Kwa wanafunzi, marufuku ya kusafiri inapunguza uwezo wao wa kupata elimu katika vyuo vya nje ya nchi. Masharti ya kuripoti mara kwa mara mahakamani au kwenye vituo vya polisi yanaweza pia kufanya iwe vigumu kubaki au kutafuta kazi au kuhudhuria masomo.19
Vizuizi vya kusafiri vinaweza pia kusababisha kutengana kwa familia. Mtetezi wa haki za binadamu alielezea kwamba vikwazo vya safari vilivyowekwa na utawala wa Nikaragua havikuwazuia tu wakimbizi wa kisiasa kurudi nyumbani – bali hatua hizo pia ziliwazuia wanafamilia kuwatembelea nje ya nchi kwa hofu kwamba wanaweza kukataliwa kurudi tena Nikaragua: "Hakuna mtu anayeweza kurudi, wala mtu anayeweza kuondoka, kwa kuhofia kwamba jambo lile lile litawapata."20 Kifo cha uraia hakifanywi tu kwa walengwa wakuu wa serikali; mtu yeyote kwenye mzunguko wao anaweza kunaswa.
- 1Human Rights Watch, “Critics Under Attack: Harassment and Detention of Opponents, Rights Defenders and Journalists Ahead of Elections in Nicaragua,” June 22, 2021, https://www.hrw.org/report/2021/06/22/critics-under-attack/harassment-a….
- 2Amnesty International, “Tunisia: Jailed opposition figures on hunger strike: Jaouhar Ben Mbarek, Khayyam Turki, Issam Chebbi, Ghazi Chaouachi, Ridha Belhaj and Abdelhamid Jelassi,” October 5, 2023, https://www.amnesty.org/en/documents/mde30/7273/2023/en.
- 3Amnesty International UK, “Tunisia: Jailed Opposition Figures on Hunger Strike,” October 5, 2023, https://www.amnesty.org.uk/urgent-actions/jailed-opposition-figures-hun…. See also interview with an activist focused on Tunisia who requested anonymity, August 2023.
- 4UN Human Rights Council, Detailed findings of the independent international factfinding mission on the Bolivarian Republic of Venezuela, A/HRC/45/CRP.11 (September 15, 2020).
- 5See, for example, interview with Nate Grubman, political scientist researching Tunisian politics, June 2023.
- 6Human Rights Watch, “To Speak Out is Dangerous: Criminalization of Peaceful Expression in Thailand,” October 24, 2019, https://www.hrw.org/report/2019/10/25/speak-out-dangerous/criminalizati….
- 7See, for example, interviews with Pavin Chachavalpongpun, a Thai scholar and activist, July 2023; Akarachai Chaimaneekarakate, advocacy lead for Thai Lawyers for Human Rights, August 2023; Tyrell Haberkorn, Director of Graduate Studies, Professor of Southeast Asian Studies, University of Wisconsin-Madison, July 2023; Kevin Hewison, Emeritus Professor, Department of Asian Studies, The University of North Carolina at Chapel Hill, July 2023; and Bencharat Sae Chua, Institute of Human Rights and Peace Studies, Mahidol University, Thailand, July 2023.
- 8Interview with a representative from the Organization against Torture in Tunisia, July 2023.
- 9Human Rights Watch, “Critics Under Attack: Harassment and Detention of Opponents, Rights Defenders and Journalists Ahead of Elections in Nicaragua,” June 22, 2021, https://www.hrw.org/report/2021/06/22/critics-under-attack/harassment-a….
- 10Human Rights Watch, “‘As Long as I am Quiet, I am Safe’: Threats to Independent Media and Civil Society in Tanzania,” October 28, 2019, https://www.hrw.org/report/2019/10/28/long-i-am-quiet-i-am-safe/threats….
- 11Alfredo Romero, “The Repression Clock: A Strategy Behind Autocratic Regimes,” Wilson Center Latin American Program, July 2020, https://www.wilsoncenter.org/sites/default/files/media/uploads/document….
- 12“País por cárcel: así secuestra el régimen de Ortega los pasaportes de los nicaragüenses [Country for prison: this is how the Ortega regime seizes the passports of Nicaraguans],” Divergentes, December 6, 2022, https://www.divergentes.com/pais-por-carcel-asi-secuestra-el-regimen-de…. See also interview with Yaritzha Mairena, representative of the National Union of Nicaraguan Political Prisoners, August 2023.
- 13Interview with a civil society actor based in Turkey who requested anonymity, July 2023.
- 14Amnesty International, “No End in Sight: Purged Public Sector Workers Denied a Future in Turkey,” May 22, 2017, https://www.amnesty.org/en/documents/eur44/6272/2017/en/; Ali Yildiz, “Turkey’s Disregard for the Freedom of Movement,” Verfassungsblog, December 11, 2019, https://verfassungsblog.de/turkeys-disregard-for-the-freedom-of-movemen….
- 15“Encarcelamientos nocturnos y juicios exprés son ‘arbitrarios y anómalos’ [Night arrests and express trials are ‘arbitrary and anomalous’],” Confidencial, May 6, 2023, https://confidencial.digital/nacion/abogada-yonarqui-martinez-anomalo-p…; “Unos 65 opositores a Ortega han sido detenidos en lo que va de mayo, según observatorio [Some 65 opponents of Ortega have been arrested so far in May, according to observations by Blue and White Monitor],” SWI swissinfo.ch, May 20, 2023, https://www.swissinfo.ch/spa/nicaragua-crisis_unos-65-opositores-a-orte….
- 16See, for example, interview with a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
- 17See, for example, interviews with Tamara Taraciuk Broner, Rule of Law Program Director for Inter-American Dialogue, August 2023; Franz von Bergen, Venezuelan journalist, June 2023; a representative from Center for Defenders and Justice, July 2023; and a Venezuelan civil society leader, August 2023.
- 18Interview with a representative from the Center for Defenders and Justice, July 2023.
- 19See, for example, interviews with Berna Akkızal, executive director and cofounder of the Civic Space Studies Association, August 2023; and a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
- 20Interview with a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
Ufuatiliaji wa karibu wa nyendo za walengwa
Wapinzani wa serikali, wa kweli na wanaodhaniwa, wamekabiliwa na aina mbalimbali za ufuatiliaji wa karibu, hasa na vyombo vya usalama. Maafisa wa polisi wanaweza kuzingira nyumba zao, kuwafuatilia wanapokuwa nje, na kuzungumza na majirani na waajiri wao. Watendaji wasio wa serikali, kama wafuasi wa serikali na wanamgambo wasio na uhusiano na serikali wanaweza pia kujihusisha na shughuli za ufuatiliaji. Vitendo kama hivyo vinalenga kuwatisha wapinzani wa kisiasa, wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, na wengine, kuwazuia wasiweze kutekeleza majukumu yao kadhalika na kuathiri maisha yao ya kawaida.
Wafungwa wa kisiasa wa Nikaragua walioachiliwa huru kwa msamaha mwaka 2019, na wale waliojihusisha na harakati kabla ya uchaguzi wa 2021, walikabiliwa na unyanyasaji huo mkubwa wa maafisa wa polisi na wafuasi wa serikali.1 Jesús Tefel, mwanaharakati aliyehojiwa na Freedom House alinukuliwa akielezea mazingira hayo:
Viongozi wakuu (wanaharakati) kila mara walisindikizwa na doria au polisi wa kitaifa kwenye magari yao, waliowafuata popote walipoenda…Haikuwa kwa dhumuni la kuwalinda. Bali ilikuwa kwa lengo la kuwakandamiza, kuwafuatilia, na hapakuwa na njia yeyote ya kuwakimbia. Kwa mfano, siku moja nilikuwa nikifatwa na pikipiki mbili, hawakuwa hata wamevaa sare za polisi. Walikuwa wamevaa kama raia. [Baadaye], ofisini kwangu kulikuwa na magari kadhaa ya polisi, na maafisa wengi wa polisi. Na wakaninyang’anya leseni yangu na kunipiga faini kwa madai ya kukimbia…Nilikaa takriban miezi mitatu au minne bila kuendesha gari kwa sababu ya kutokuwa na leseni. Kwa hiyo ilikuwa ngumu sana kujificha. Nyumba za viongozi zililindwa mda wote, bila kificho chochote, huku umma mzima ukishuhudia…. Wanaulizia kitambulisho chako. Wanakuuliza wapi unakwenda, wapi ulipotoka, na nani aliyekuona.2Wengi wa wanaharakati wanafunzi walioshiriki katika maandamano ya kudai demokrasia ya mwaka 2020/21 nchini Thailand walikabiliwa na ufuatiliaji mkali wa polisi, wakiwemo wale waliokamatwa na kuachiliwa kwa dhamana. Kevin Hewison, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mtaalam wa demokrasia nchini Thailand, alibainisha kuwa “imekuwa kawaida kwa polisi kuweka kambi nje ya makazi ya wanaharakati, wakijitokeza mara kwa mara kuwaangalia, kuwahoji majirani ili kuhakikisha walengwa wanapata shinikizo la kijamii la kuacha shughuli zao.”3 Miongoni mwa wale walioathirika ni vijana wadogo, ambao wamekuwa wakikabiliwa na ufuatiliaji wa mara kwa mara ambao, Akarachai Chaimaneekarakate, kiongozi wa utetezi wa Wanasheria wa Haki za Kibinadamu wa Thai anasema, “Ni kawaida sana, ukweli ni kwamba, washtakiwa wote hawa wangeniambia hadithi ile ile: ‘…. Ninaona mtu mwenye fulana nyeupe na mtindo fulani wa nywele. Ndio, huyo dhahiri ni afisa wa polisi aliyevaa nguo za kiraia.’ Wanajifunza kutambua maafisa wa polisi waliovaa kiraia.”4 Vifaa vya ufuatiliaji vya kielektroniki pia viliunganishwa kwa wanaharakati wa Thailand walioachiwa kwa dhamana kipindi hiki.5
Hata bila mashtaka, wapinzani huitwa kwa mahojiano ya mara kwa mara yanayokusudiwa kufuatilia na kuwatisha. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Nate Grubman, akizungumzia kiongozi wa upinzani wa Tunisia aliyefungwa gerezani, Rached Ghannouchi,6 anaeleza kuwa: "Kabla ya kukamatwa kwake, ilionekana kama kila wiki alikuwa akiitwa mahakamani kwa kosa x, angetumia siku nzima kujibu maswali na kisha wangemrudisha nyumbani mwishoni mwa siku. Yeye ni mzee. Ninafikiria kwamba huo ni mzigo mzito. Itakuwa ni mzigo kwa mtu yeyote”.7
Vitisho vya ufuatiliaji wa kiusalama, na uvamizi kwenye makazi na kwenye maeneo ya kazi imewalazimisha kubadili mienendo yao, ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari za usalama wao. Nchini Tanzania, Fulgence Massawe, mkurugenzi wa utetezi na mageuzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, alishiriki kuelezea huku akionyesha kadi za ofisi yake: “Tulizoea kufanya kazi kwa uhuru, lakini kwa sasa tunatumia vifaa na kadi za kielektroniki zinazoweza kufuatiliwa kwa urahisi.”8 Uvamizi wa majumbani nchini Uturuki umekuwa jambo la kawaida kwa baadhi ya wapinzani wa serikali kiasi kwamba hujiandaa kwa ajili ya tukio hilo. Banu Tuna, mwandishi na mwanaharakati wa Kituruki, alielezea kuwa maafisa wa polisi mara nyingi hufanya uvamizi siku za Ijumaa asubuhi ili walengwa watumie wikiendi kizuizini; alimuelezea mmoja wa watendaji wa asasi za kiraia ambaye hupanga majukumu yake kuzingatia ratiba hiyo.9
Ufuatiliaji huu wa wazi unatengeneza shinikizo la kijamii, unazuia uhuru wa kusafiri, na unachochea mzigo mkubwa wa kisaikolojia. Kwa mfano, Eric Goldstein, naibu mkurugenzi wa Kitengo cha Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika Shirika la Human Rights Watch, alibainisha kwamba wale wanaokumbana na sharti la kuhudhuria polisi mara kwa mara nchini Tunisia wanakabiliwa na mazingira ya kutengwa na jamii zao, "si kwa sababu majirani walidhani mtu huyo alikuwa amefungwa kwa haki, bali kwa sababu walitaka kuepuka mawasiliano yoyote ambayo yangewatia shaka wao wenyewe."10 Mtendaji wa asasi ya kiraia nchini Tanzania, akisimulia uzoefu wake mwenyewe, alisema: "Wanahakikisha kwamba haupati utulivu wa kuendelea na shughuli zako."11
Kama ilivyo mbinu zingine zinazopelekea kifo cha uraia, udhibiti na ufuatiliaji wa karibu unaongeza ugumu kwa wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa upinzani, na wadau wengine katika kupigania kuleta mabadiliko ya kidemokrasia na kulinda haki za binadamu. Akizungumzia hali ya kisiasa nchini Venezuela chini ya utawala wa Rais Maduro, mwanazuoni mmoja alisema: "Nafikiri kwa sasa... wanaharakati maarufu na wenye ushawishi hasa wale kutoka asasi za kiraia au vinara wa harakati... huhisi kuwa wanafuatiliwa kila wakati, kiasi cha kwamba wanapaswa kufikiria kila kitu wanachokifanya hata mara kumi na kuhakikisha hawavuki mipaka dhidi ya serikali."12 Mtendaji wa asasi ya kiraia, akizungumzia shughuli za mitandao ya kijamii nchini Uturuki, alisema: "Nusu ya fikra zako unasema, oh, nitakuwa salama. Hawatonifuatilia. Huku nusu nyingine ya fikra zako ikisema, endapo watanifuatilia, basi maisha yangu yapo hatarini."13
Kuzuia upatikanaji wa fursa za Ajira, elimu na manufaa ya serikali
Wapinzani wa kisiasa, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wanasiasa waliotumikia utawala wa zamani, na wanachi wa kawaida ni miongoni mwa watu wanaokutana na vikwazo vya kisiasa katika ajira na elimu, kuondolewa manufaa ya kijamii, na wakati mwingine kunyimwa uraia. Aina hii ya hujuma inaongezeka kwa kasi kubwa kwenye sekta ya umma, ingawa pia shinikizo la kijamii linaweza kuathiri uwezo wa watu kushiriki kwenye sekta binafsi.
Kuorodheshwa kwenye orodha ya watu hatari kwa kutumia mfumo kumesababishwa na kuongezeka kwa kasi ya mmomonyoko wa kidemokrasia. Kama ambavyo rais wa zamani Chávez alipobadilisha utaratibu uliozoeleka wa jamii ya Venezuela, "Hofu...ilikuwa unaweza kuwekwa kwenye orodha ya watu hatari na kupelekea kupoteza fursa za kupata kazi au kupewa huduma za serikali,” alisema Javier Corrales, mchambuzi wa masuala ya kisiasa.14 Jitihada za kuwaondoa Chávez na Maduro kwenye madaraka ya Urais mwaka 2004 zilipelekea watu wengi kufutwa kazi sambamba na kuwekwa kwenye orodha ya watu hatari. Kwa mfano, mwanasiasa ambaye ni mfuasi wa serikali, Luis Tascón, alichapisha mtandaoni orodha ya watu waliokuwa wametia saini maombi husika, yaliyokusanywa na Baraza la Taifa la Uchaguzi, kwa agizo la Chavez. Chapisho hilo liliojulikana kama orodha ya Tascón, iliongoza maamuzi ya kuwafuta kazi na kuwaorodhesha kwenye orodha ya watu hatari watumishi wa serikali na mashirika yanayomilikiwa na serikali.15 Zoezi hilo la kufukuza kazi watumishi wa serikali lilifanyika pia baada ya jaribio la kumwondoa Rais Maduro madarakani mwaka 2016.16 Huko nchini Nikaragua, watumishi wa umma wakiwemo wafanyakazi wa huduma za afya, walimu, na wahadhiri wa vyuo vikuu walifutwa kazi kwa kuhusika katika maandamano ya kupinga serikali ama kwa kusaidia washiriki wa maandamano hayo ya mwaka 2018.17
Nchini Uturuki, kundi la wasomi zaidi ya elfu moja wanaojulikana kama Wanazuoni wa Amani walitia saini waraka wa wazi mwezi Januari 2016 wakielezea kuunga mkono amani na kuunga mkono Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) kilichopigwa marufuku na serikali. Matokeo yake walifutwa kazi na kuzuiwa kufanya kazi katika sekta ya umma.18 Katika kujibu barua yao, mwandishi wa habari anayeunga mkono serikali aliomba “hukumu ya kifo cha uraia” itumiwe kuwaadhibu watu hao, ikiwa ni pamoja na jamii kuwatenga.19 Miezi michache baadae, kufuatia jaribio la mapinduzi, zaidi ya wafanyakazi 100,000 wa sekta ya umma walifutwa kazi bila kufuatwa kwa utaratibu kwa amri mbalimbali za serikali,20 kwa madai ya kuhusishwa na Shirika la Kigaidi la Fetullahist (FETÖ), kikundi cha kigaidi ambacho kilishutumiwa na serikali kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi. Kama ilivyotokea kwa kundi la Wanazuoni wa Amani, wafanyakazi hao walizuiliwa kufanya kazi katika sekta ya umma, hati zao za kusafiria zilibatilishwa, na hawakuweza kupata mafao yao ya huduma za afya.21 Watumishi hao waliitwa hadharani kama wafuasi wa FETÖ, kitu ambacho kilihatarisha usalama na uhuru wao wa kutembea, na kungeweza kusababisha kukamatwa tena.22
Nchini Nicaragua, wafungwa wa kisiasa walioachiliwa kwa msamaha hawakuweza kurudi vyuoni, kwa sababu rekodi zao zilifutwa, na walipata ugumu wa kutafuta ajira kutokana na unyanyapaa wa kijamii. Mtetezi mmoja wa haki za binadamu alikumbuka kisa kimoja ambacho mtu aliyepewa msamaha "hakuruhusiwa hata kufanya kazi ndogondogo kwenye jumuiya yao. Alikwenda kutafuta kibarua cha kufua nguo au kibarua cha kupiga pasi nguo…. na watu waliomwajiri wakamwambia asingeweza tena kufanya kazi hizo kwa sababu yeye amehusika kupanga njama ya mapinduzi ya kuiondoa serikali.”23 Wafungwa wa zamani wa kisiasa waliohusishwa na maandamano ya hivi karibuni ya kudai demokrasia nchini Thailand, wamekabiliwa na mashtaka mbalimbali, shinikizo kubwa la kijamii na changamoto ya kupata ajira na kuhudhuria masomo.24 Baadhi ya waliohojiwa nchini Uturuki walibanisha unyanyapaa kama huo kwa walengwa: “Hata unapotoka gerezani, alama yake huondoka nawe”, alisema mwanazuoni mmoja wa Kituruki.25
Ubaguzi katika ugawaji wa rasimali za serikali hupelekea pia kifo cha uraia. Mwaka 2017, serikali ya Venezuela ilizindua kadi ya kitambulisho, kilichofahamika kama carnet de la patria, au kadi ya utaifa, iliyounganishwa na huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali kwa njia mtandao kama pensheni, matibabu, na chakula.26 Bwana Hernandez-Roy alibainisha kuwa kitambulisho hicho kimekuwa “kikitumika kama silaha... ambapo wanaweza kufuatilia mienendo yako," na ikiwa mtu ameonekana kama mpinzani "hautofanikiwa kupata ruzuku ya chakula.”27 Nchini Tunisia, baadhi ya mahakimu, wabunge, pamoja na watu wengine waliofutwa kazi kiholela na Rais Saïed, wameachwa bila bima ya afya, kitendo ambacho ni hatari kwa sababu wengi wao ni wazee na wana changamoto za kiafya.28
Wanafamilia pia wamekabiliwa na aina mbalimbali ya kifo cha uraia. Nchini Nikaragua, hatua za serikali ya kuwavua uraia wapinzani na wakosoaji zilikuwa na athari kubwa kwa ndugu wa wahanga. Watoto wa walengwa wameripotiwa kunyimwa huduma za matibabu, udahili wa masomo, na pasipoti.29 Katika baadhi ya matukio, serikali iliwaondolea ubini wa jina la mzazi kwenye rejesta ya raia, watoto wa wazazi waliolengwa.30 Nchini Tanzania, watoto wa wanachama wa upinzani wanakabiliwa na ugumu kupata fursa serikalini, kama vile mikopo ya vyuo vikuu. Mwanazuoni mmoja alishiriki kusimulia kisa cha mtoto mmoja aliyenyimwa mkopo wa chuo kwa sababu ya msimamo wa kisiasa wa wazazi wake: "Walikuwa wakisema, oh, hakuna wino wa muhuri. Na hata aliporudi na wino, walisema kwamba, huu si wino rasmi wa serikali, hivyo hatutoweza kutumia wino huu."31 Akisisitiza uwekaji kwenye orodha ya watu wasiostahili kupata fursa serikalini, mwanazuoni huyo aliongezea kwamba: "Kuna hizi aina zote za maeneo ambayo unaweza kuwanyima watu ufikiaji wa huduma za msingi ambazo wanastahili kisheria.”32
Ingawa kifo cha uraia kinaweza kutokea hatua kwa hatua, matokeo ya mbinu za ukandamizaji yanaongezeka kadiri mda unavyokwenda mbele. Tukio baya na la ghafla lilitokea Februari 2023, wakati jopo la majaji watatu walipowavua raia 317 wa Nikaragua urai wao, ikiwemo wafungwa 222 wa kisiasa waliokuwa wameachiliwa huru na kupelekwa Marekani. Uamuzi huo ulihalalishwa kisheria kupitia mageuzi ya sheria ambayo yaliruhusu mamlaka husika kufuta uraia wa wale walioonekana na serikali kuwa wasaliti. Miongoni mwa walioathiriwa ni waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu, viongozi wa mashirika ya kiraia, viongozi wa upinzani, na maafisa wa serikali.33 Wahanga hawa wanakabiliwa na changamoto ya kuanzisha upya maisha yao katika nchi ya kigeni huku wakifikiria mazingira mabaya ya uhamisho wao. Hali hii imekuwa ni mapambano kwa wengi, na, "kidogo kidogo", alisema mwanasheria wa haki za binadamu, "wanapoteza shauku ya kile kinachotokea nchini Nikaragua.”34
- 1Amnesty International, “Silence at any cost: State tactics to deepen the repression in Nicaragua,” February 15, 2021, https://www.amnesty.org/en/documents/amr43/3398/2021/en/; Human Rights Watch, “Critics Under Attack: Harassment and Detention of Opponents, Rights Defenders and Journalists Ahead of Elections in Nicaragua,” June 22, 2021, https://www.hrw.org/report/2021/06/22/critics-under-attack/harassment-a….
- 2Interview with Jesús Tefel, Nicaraguan activist, July 2023.
- 3Interview with Kevin Hewison, Emeritus Professor, Department of Asian Studies, The University of North Carolina at Chapel Hill, July 2023.
- 4Interview with Akarachai Chaimaneekarakate, advocacy lead for Thai Lawyers for Human Rights, August 2023.
- 5See, for example, interviews with Pavin Chachavalpongpun, Thai scholar and activist, July 2023; Akarachai Chaimaneekarakate, advocacy lead for Thai Lawyers for Human Rights, August 2023; Tyrell Haberkorn, Director of Graduate Studies, Professor of Southeast Asian Studies, University of Wisconsin-Madison, July 2023; Kevin Hewison, Emeritus Professor, Department of Asian Studies, The University of North Carolina at Chapel Hill, July 2023; and a Thai civil society actor, August 2023.
- 6Amnesty International, “Tunisia: Ghannouchi sentencing marks aggressive crackdown on Saied opposition,” May 18, 2023, https://www.amnesty.org/en/latest/news/2023/05/tunisia-ghannouchi-sente….
- 7Interview with Nate Grubman, political scientist researching Tunisian politics, June 2023.
- 8Interview with Fulgence Massawe, director of advocacy and reforms for the Legal and Human Rights Centre, July 2023.
- 9Interview with Banu Tuna, Turkish journalist and activist, August 2023.
- 10Interview with Eric Goldstein, Deputy Director, Middle East and North Africa Division, Human Rights Watch, August 2023.
- 11Interview with a Tanzanian civil society actor who requested anonymity, July 2023.
- 12Interview with a scholar focused on Venezuela, August 2023.
- 13Interview with a Turkish civil society actor, June 2023.
- 14Interview with Javier Corrales, Dwight W. Morrow 1895 professor of Political Science, Amherst College, August 2023.
- 15Human Rights Watch, “A Decade Under Chávez: Political Intolerance and Lost Opportunities for Advancing Human Rights in Venezuela,” September 2008, https://www.hrw.org/reports/2008/venezuela0908/index.htm; Transparencia Venezuela, “Carnet de la Patria: El Apartheid Revolucionario [Homeland Card: Revolutionary Apartheid],” https://transparenciave.org/wp-content/uploads/2018/03/Carnet-de-la-pat….
- 16Mariana Zuñiga, “Venezuelan civil servants signed a petition to oust the president. Now they’re losing their jobs,” Washington Post, July 23, 2016, https://www.washingtonpost.com/news/worldviews/wp/2016/07/23/venezuelan….
- 17Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights, “Human Rights Violations and Abuses in the Context of Protests in Nicaragua 18 April - 18 August 2018,” August 2018, https://www.ohchr.org/sites/default/files/Documents/Countries/NI/HumanR….
- 18Frontline Defenders, “Judicial Harassment against the Members of Academics for Peace,” last updated November 8, 2019, https://www.frontlinedefenders.org/en/case/judicial-harassment-academic….
- 19Cem Küçük, “‘Medeni Ölüm’ mekanizmaları! [‘Civil death’ mechanisms!],” Star, January 16, 2016, https://www.star.com.tr/yazar/medeni-olum-mekanizmalari-yazi-1082729/.
- 20Ali Yildiz, “Turkey’s Disregard for the Freedom of Movement,” Verfassungsblog, December 11, 2019, https://verfassungsblog.de/turkeys-disregard-for-the-freedom-of-movemen….
- 21Amnesty International, “No End in Sight: Purged Public Sector Workers Denied a Future in Turkey,” May 22, 2017, https://www.amnesty.org/en/documents/eur44/6272/2017/en/.
- 22Ibid.
- 23Interview with a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
- 24Thai Lawyers for Human Rights, “1 Year of Political Bails: At Least 54 Required to Wear EM Devices Affecting Their Daily Lives,” April 25, 2022, https://tlhr2014.com/en/archives/42865. See also interviews with Pavin Chachavalpongpun, Thai scholar and activist, July 2023; Akarachai Chaimaneekarakate, advocacy lead for Thai Lawyers for Human Rights, August 2023; Tyrell Haberkorn, Director of Graduate Studies, Professor of Southeast Asian Studies, University of Wisconsin-Madison, July 2023; Kevin Hewison, Emeritus Professor, Department of Asian Studies, The University of North Carolina at Chapel Hill, July 2023; a Thai civil society actor, August 2023; and a civil society actor focused on Thailand who requested anonymity, June 2023.
- 25Interview with a Turkish academic who requested anonymity, July 2023.
- 26Freedom House, “Venezuela,” in Freedom on the Net 2023, https://freedomhouse.org/country/venezuela/freedom-net/2023; Transparencia Venezuela, “Carnet de la Patria: El Apartheid Revolucionario [Homeland Card: Revolutionary Apartheid],” https://transparenciave.org/wp-content/uploads/2018/03/Carnet-de-la-pat….
- 27Interview with Christopher Hernandez-Roy, Senior Fellow and Deputy Director, Americas Program, Center for Strategic and International Studies, August 2023.
- 28See, for example, interview with Nate Grubman, political scientist researching Tunisian politics, June 2023.
- 29See, for example, interview with a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
- 30Noel Pérez Miranda, “Ortega quita apellido a hijos de exreos políticos desterrados; a otros les niega entrega de pasaporte [Ortega removes last names from children of exiled former political prisoners; others are denied passports],” Artículo 66, March 4, 2023, https://www.articulo66.com/2023/03/04/ortega-quita-apellido-hijos-exreo…. See also interview with a Nicaraguan human rights defender, August 2023.
- 31Interview with a scholar focused on Tanzania who requested anonymity, August 2023.
- 32Ibid.
- 33“Despojan de nacionalidad y derechos ciudadanos, y confiscan a 94 nicaragüenses [Ortega strips 94 Nicaraguans of nationality and citizen rights],” Confidencial, February 16, 2023, https://confidencial.digital/nacion/despojan-de-nacionalidad-y-derechos…; US Department of State, “Sanctioning Three Nicaraguan Judges Involved in Depriving Nicaraguans of Their Basic Right to Citizenship,” April 19, 2023, https://www.state.gov/sanctioning-three-nicaraguan-judges-depriving-nic….
- 34Interview with a Nicaraguan human rights lawyer who requested anonymity, August 2023.
Udhibiti wa Mali
Mbinu nyingine inayopelekea kifo cha uraia ni kudhibiti wapinzani na wakosoaji wa serikali kumiliki mali zao, na hivyo kuzuia uwezo wao wa kujihifadhi kwenye makazi yao na ustawi wao wa kifedha. Mara nyingi, mbinu hii hutumiwa pamoja na mbinu zingine zilizojadiliwa. Mbinu hizi, kukamata au kufungia akaunti za benki na kunyang’anya mali za walengwa zinaweza kutumika pamoja kwenye uchunguzi wa jinai, ukamataji, au masharti ya kuachiliwa huru, au zinaweza kutumika kwa kujitegemea.
Wafungwa wa kisiasa wanaodhaniwa kukiuka sheria ya Venezuela ya dhidi ya uhalifu uliopangwa na Ufadhili wa Ugaidi, wanaweza kunyang’anywa mali zao kisheria, mara nyingi ikiwa ni baada ya kuondoka au kukimbia nchi: "Unaweza kuona nyumba na ofisi nyingi kote nchini ambapo polisi... maafisa wa ujasusi... hutumia kibinafsi, kwa faragha", alisema kiongozi wa asasi za kiraia nchini Venezuela, akizungumza juu ya mali zilizokamatwa na serikali.1 Mamlaka za Venezuela pia zimefunga akaunti za benki za wapinzani na kushikilia mali na biashara kwa ujumla.2 Kama mbinu nyinginezo, kukamata mali na kufungia akaunti za benki kunaweza kutumika dhidi ya familia za wahanga.3
Mtendaji mmoja wa asasi za kiraia nchini Tanzania alipoteza kampuni yake baada ya kukabiliwa na mashtaka ya jinai yasiyo na msingi, pamoja na hatua zingine zinazopelekea kifo cha uraia:
Sikuruhusiwa kuvuka mipaka ya Dar es Salaam. Pasipoti yangu ilichukuliwa. Akaunti zangu binafsi za benki zilifungwa. Nilikuwa na biashara yenye faida. Sasa hiki ndicho walichokifanya .... Wanahakikisha kwamba huwezi kufanya biashara. Sikuwa tena nikipata mapato kwa sababu walifanikiwa kuwafikia watu wote niliokuwa nafanya nao kazi, wasambazaji wangu, yeyote...waliwatisha [wao] na wote waliacha kufanya kazi na mimi. Kampuni niliyokuwa namiliki ilichukuliwa na baadhi ya watu kutoka chama tawala bila mimi kusaini hati yoyote. Hivyo nikajikuta si mkurugenzi katika kampuni yangu mwenyewe. Nilijikuta si mbia wa kampuni yangu mwenyewe.4
Mbali na zoezi la kuwavua uraia zaidi ya wananchi 300 wa Nikaragua, mwezi Februari 2023, majaji waliamuru mali zao zitaifishwe. Serikali ilitaifisha nyumba na mashamba huku ikifuta majina ya wamiliki kutoka kwenye orodha ya wamiliki mali, na kisha benki zikafunga akaunti za wahanga hao. Ndugu na wapangaji wanaoishi katika majengo yaliyotaifishwa, walilazimishwa kulipa kodi kwa ofisi ya mwanasheria mkuu.5 Utaifishaji wa mali umeripotiwa kuenea zaidi ya wale waliovuliwa uraia. Mwandishi wa habari wa Nikaragua alisema: “Kuna watu ambao hawajashtakiwa kwa uhaini lakini ni wapinzani, lakini nyumba zao zimepotea kwenye orodha ya usajili wa mali. Yaani, ni siku moja tu unabaki bila chochote. Akaunti zako za benki zinafungwa, na benki haikupi hata taarifa ya awali.”6
Kufungwa kwa akaunti ya benki kunasababisha matatizo makubwa hasa kwa wale wanaokabiliana na changamoto za kiuchumi. Akizungumzia kuhusu hali nchini Tunisia, Radwan Masmoudi, rais wa Kituo cha Mafunzo ya Uislamu na Demokrasia, alieleza kwamba: “Watu wanateseka sana. Uchumi ni mbaya sana. Kuna upungufu mkubwa wa chakula. Halafu juu ya hayo, wanafungia akaunti zako za benki, je utaishi vipi?7
Vitisho vya kudumu vya kifo cha uraia
Miongoni mwa hali zinazosababisha kifo cha uraia, iwe ni marufuku ya kusafiri, kufuatiliwa na polisi, kufutiwa rekodi za kitaaluma, au kunyimwa pensheni, ni hofu ya kwamba mlengwa anaweza kupelekwa gerezani wakati wowote. Maelezo ya kawaida miongoni mwa wale waliohojiwa na Freedom House ni kwamba, mara nyingi mashtaka ya jinai hayasuluhishwi kikamilifu, na hivyo kuacha wazi uwezekano wa kukamatwa tena. Vikwazo kwenye ushiriki wa kawaida katika jamii, pamoja na tishio endelevu la kuwa mfungwa wa kisiasa, vimesababisha wapinzani wa serikali kukimbia nchi. Matokeo ya kifo cha uraia pi yanaweza kutumika kama onyo kwa wengine.8
Kifo cha uraia huzuia mabadiliko ya kidemokrasia kwa sababu kinaweza kusababisha watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, viongozi wa upinzani, na wengine kuacha majukumu yao ya msingi. Akarachai, kutoka Taasisi ya Wanasheria wa Haki za Binadamu Thailand, alisema: “Viongozi wengi wa waandamanaji wameelemewa na masharti mengi ya dhamana na tunahisi kwamba wengi wao wamechoka sana. Mateso haya ya kila mara kutoka kwa mahakama, masharti ya dhamana... kwa kweli huwachosha na hupelekea wengi wao kutojihusisha sana na siasa.”9 Berna Akkızal, mkurugenzi mtendaji na mwanzilishi mwenza wa Chama cha Mafunzo ya Nafasi ya Raia nchini Uturuki, alielezea hali kama hiyo: “Nadhani, watu huzoea vitu kama hivyo. Watu huzoea uonevu. Mimi kama mwanaharakati, hii ndio sehemu ngumu zaidi kwangu.”10
Mbinu za hila zaidi zinazopelekea kifo cha uraia, ikilinganishwa na vifungo va kisiasa, huongeza ugumu kwa wadau wa nje kutambua wakati gani kifo cha uraia kinatokea na jinsi kinavyozuia demokrasia na kazi ya haki za binadamu. Kutambua mbinu zinazosababisha kifo cha uraia, na kuelewa athari zake kwa walengwa haswa juu ya afya ya mwili na akili, ustawi wa kiuchumi, na, kimsingi, uwezo wa kushiriki katika jamii, ni muhimu katika kupunguza na kurudisha nyuma mmomonyoko wa kidemokrasia.
- 1Interview with a Venezuelan civil society leader, August 2023.
- 2Interview with Christopher Hernandez-Roy, Senior Fellow and Deputy Director, Americas Program, Center for Strategic and International Studies, August 2023.
- 3Alfredo Romero, “The Repression Clock: A Strategy Behind Autocratic Regimes,” Wilson Center Latin American Program, July 2020, https://www.wilsoncenter.org/sites/default/files/media/uploads/document….
- 4Interview with a Tanzanian civil society actor who requested anonymity, July 2023.
- 5Organization of American States, “Nicaragua: IACHR and REDESCA Express Concern About Violations of Property and Social Security Rights,” April 14, 2023, https://www.oas.org/en/IACHR/jsForm/?File=/en/iachr/media_center/PRelea….
- 6Interview with a Nicaraguan journalist, July 2023.
- 7Interview with Radwan Masmoudi, president of the Center for the Study of Islam and Democracy, August 2023.
- 8See, for example, interview with Jesús Tefel, Nicaraguan activist, July 2023.
- 9Interview with Akarachai Chaimaneekarakate, advocacy lead for Thai Lawyers for Human Rights, August 2023.
- 10Interview with Berna Akkızal, executive director and cofounder of the Civic Space Studies Association, August 2023.
Mashambulizi dhidi ya Uhuru wa Mahakama na ufinyu wa kupata msaada wa kisheria
Matokeo muhimu ya utafiti uliofanywa katika nchi sita tofauti na ambao una madhara katika demokrasia inayopingwa ulimwenguni kote, ni jukumu kuu la Mahakama inayotii. Sambamba na hilo, mbali ya kuwa kiwezeshi cha vifungo vya kisiasa na kifo cha uraia, kupungua kwa uhuru wa mahakama kwa kiasi kikubwa kumewapunguzia wahanga wa ukandamizaji wa haki, fursa ya kutafuta msaada wa kisheria na uwajibikaji. Wakati huo huo, katika mazingira ya utawala wa kiimla, watumishi wa mahakama wanaweza kugeuka kuwa wafungwa wa kisiasa na wahanga wa kifo cha uraia (kunyang’anywa haki zote za kiraia), yote hayo ni kutokana na kupungua kwa uhuru wa mahakama katika utekelezaji wa majukumu yake kama moja ya mihimili mikuu ya dola.
Kwa mujibu wa kesi mbalimbali zilizofuatiliwa kwa ukaribu na shirika la Freedom House, viongozi walioshinda chaguzi hivi karibuni na ambao wana viashiria na matamanio ya udikteta, wanapanga kupindua mfumo wa mahakama ili ufanye kazi kwa manufaa yao. Kabla ya kuwa Rais wa Nikaragua mwaka 2007, Daniel Ortega kwa kushirikiana na Rais wa wakati huo Arnoldo Alemán, aliweza kupata idadi ya kutosha ya watumishi wa mahakama wa mrengo wake atakaowateua ili wafanye kazi katika mahakama ya juu zaidi. Mahakama pia iliwabakisha kazini majaji ambao walikuwa na ushirika na Rais Ortega hata kabla ya makubaliano na Rais Arnoldo.1 Wakati wa maandamano ya kupinga serikali ya mwaka 2018 yalipoibuka, mahakama tiifu kwa serikali ya kidikteta tayari ilikuwepo hatamuni na ilitumika kama mwezeshaji muhimu wa vizuizi, hukumu na vifungo vya kisiasa kwa wapinzani na wakosoaji wa serikali.2
Hali kama hii pia imedhihirika huko nchini Venezuela. Baada ya Rais Hugo Chávez kuingia madarakani mnamo mwaka 1999, alipata mamlaka rasmi na nguvu ya kuwaondoa majaji wote na kuunda upya mfumo wa mahakama kwa kupitia vyombo vya kutunga sheria ambavyo vilivyokuwa chini yake kwa kiasi kikubwa. Vyombo hivi vilifanya kazi kwa kupitia tume za dharura kuwaondoa au kuwasimamisha majaji kwa kuwahusisha na madai ya uongo na yasiyoeleweka juu ya upokeaji Rushwa na baadaye vikadhibiti mahakama kuu. Kwa kuwa mahakama kuu ndio inayosimamia teuzi katika mahakama za chini, mfumo mzima wa mahakama ulizidi kupungukiwa na uhuru.3 Mageuzi ya mfumo wa mahakama wa Venezuela uliofanywa na Chávez, ulipelekea ukandamizaji mkubwa ambao ulianza chini ya utawala wa Rais Maduro mnamo mwaka 2014,4 vile vile kulichangia kupungua kwa njia halali za wananchi na wakosoaji wa serikali kukimbilia na kutafuta msaada wa kisheria.
Katika hali sawa ana hiyo, Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Bw. Erdoğan alidhoofisha uhuru wa mahakama nchini humo. Udhaifu wa mfumo wa mahakama ambao tayari ulikuwa na sura ya kisiasa, uliimarishwa zaidi mnamo mwaka 2010 kwa kupitia kura ya maoni juu ya marekebisho ya katiba, mchakato uliomwezesha Rais Erdoğan kuweza kuunda upya mfumo wa mahakama. Mabadiliko hayo ya mfumo yalipelekea hukumu zisizokuwa na msingi kwa raia na taasisi zilizoonesha kupinga na kutounga mkono chama cha Justice and Development Party (AKP).5 Kura nyingine ya maoni ya marekebisho ya katiba ya mwaka 2018, ilimpa Rais Erdoğan mamlaka zaidi ya kuteua watumishi wa muhimili wa mahakama.6 Maamuzi ya mahakama yaliyowapa ushindi upande wa washtakiwa hayakuwa na nguvu yeyote katika utekelezaji, hii kwa mfano, inajumuisha maamuzi ya mahakama ya mwaka 2019, ambayo iliondoa adhabu na kulinda uhuru wa kujieleza kwa Wanazuoni wa Amani: Licha ya ushindi huo, bado wanachama wengi wa kundi hilo waliendelea kukumbana na viashiria vya kifo vya uraia. Kwa mfano, baadhi ya walishindwa kupata kazi katika vyuo vya elimu ya juu, kwa sababu Rais Erdoğan alikuwa ameteua wakuu wa vyuo walio upande wa serikali na ambao hawakuwa tayari kuajiri wanataaluma wakosoaji wa serikali.7
Nchini Tunisia, Rais Saïed baada tu ya kulivunja bunge mnamo mwaka 2021, aliendelea na kuvunja baraza kuu la Mahakama na badala yake kuunda chombo za mpito ambacho watumishi wake waliteuliwa na kufanya kazi kwa amri ya rais.8 Rais Saïed, baadae alitoa na kupitisha amri ya rais ambayo ilimpa mamlaka ya kumuondoa jaji yeyote bila ya kufuata taratibu zilizopo za sheria. Aliweza kuwafuta kazi majaji 57 kwa tuhuma za rushwa na ukosefu wa maadili katika kazi zao.9 Ingawa mahakama ya Kiutawala ya Tunis ilisimamisha amri ya kufutwa kazi kwa majaji 47 miongoni mwao, Wizara ya Sheria nchini humo imekataa kuwarejesha kazini majaji hao.10 “Katika uhalisia wa mambo taasisi hazipo tena,” alieleza mfungwa wa zamani wa kisiasa nchini Tunisia. Aliendelea kueleza, “(Sisi) tunao majaji ambao wanaogopa kuamua kesi… Jamii inapokosa haki, inakuwa ni jamii iliyopotoka na kuharibika”.11
Mahakama za kijeshi na mahakama mahsusi, ambazo kwa namna moja zimekuwa zikizuia haki ya kufuata utaratibu wa kisheria katika uendeshaji wa kesi, zimekuwa pia zikitumika dhidi ya wale wanaopinga na kukosoa serikali. Kwa mfano, kesi za kisiasa nchini Venezuela, zinaweza kuendeshwa katika mahakama za kijeshi au mahakama mahsusi za kesi za ugaidi.12 Kwa mda mrefu baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2014 nchini Thailand, baadhi ya makosa kama vile uhaini, kuhamasisha uasi dhidi ya serikali, na kukiuka amri na maelekezo ya utawala wa kijeshi, yalisikilizwa na kuamuliwa katika mahakama za kijeshi.13
Majaji wa mahakama wako katika hatari ya kuwa walengwa wa mifumo kandamizi ya ki-mahakama iliyotekwa kimabavu na viongozi wenye viashiria na matamanio ya udikteta. Kwa mfano, kufuatia jaribio la mapinduzi nchini Uturuki mwaka 2016, serikali iliwaondoa zaidi ya majaji na waendesha mashtaka 4,000,14 na wengine zaidi ya 2,000 waliwekwa kizuizini kwa kutuhumiwa kuhusika katika kula njama au kuwa na uanachama katika makundi ya kigaidi.15 Wawili kati ya mahakimu 57 walioondolewa kazini nchini Tunisia, walikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa miezi bila ya kuhukumiwa.16 Jitihada za kupinga mashambulizi dhidi ya uhuru wa mahakama, zimekumbana na adhabu ya dola. Kwa mfano, jaji mmoja nchini Tunisia aliposaidia kuandaa mgomo uliolenga kupinga uondolewaji kazini kiholela, Baraza Kuu la Mpito la Mahakama lilimuondolea kinga yake kama jaji na kisha uchunguzi wa makosa ya kijinai ulifunguliwa dhidi yake, kwa tuhuma ya kufanya uchochezi.17
Nchini Venezuela, Jaji mmoja aitwaye María Lourdes Afiuni alinyang’anywa uhuru wake kwa muda mrefu, kesi ambayo ilitumika kama onyo kwa majaji wengine, kuwa wana ulinzi mdogo sana kuepuka adhabu kali na za mara moja kutoka katika mamlaka.18 Mwaka 2009, Afiuni akiwa jaji, aliamuru na kusimamia kuachiwa kwa mtumishi wa benki aliyetuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kifedha. Mtumishi huyo alikuwa amewekwa kizuizini kwa muda mrefu bila kuhukumiwa, kinyume na muda wa kisheria wa kumuweka mtu kizuizini. Baadae mfanyakazi huyo wa benki alikimbia nchi yake. Punde baada ya kutoa maamuzi hayo, Afiuni alikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa kuhusishwa na tuhuma za rushwa. Kisha baada ya miaka miwili kizuizini, alihamishwa na kuwekwa kizuizi cha nyumbani, kabla ya kuachiwa baadae kwa masharti ya kutoondoka Venezuela, ikiwa ni moja ya hatua ya kumdhibiti. Mwaka 2019, alihukumiwa kwenda jela miaka mitano.19 (Japo bado hajaanza kutumikia kifungo hicho).
Katika mgongano mkubwa kati ya Mahakama Kuu za Uturuki, Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kikatiba wa Novemba 2023, wa kumuachia huru Bw. Can Atalay, Mwanasheria na Mbunge ambaye amekuwa kizuizini tangu Aprili 2022. Mahamaka ya Rufaa haikuishia hapo, ilienda mbali zaidi na kufungua mashtaka ya kijinai dhidi ya watumishi wote wa Mahakama ya Kikatiba walioshiriki kuamua na kutoa uamuzi wa kuachiwa kwa Bw. Atalay.20 Kwa nyakati tofauti, katika nchi za Venezuela na Tanzania, majaji ambao wamekuwa wakikinzana na mamlaka wamekuwa wakihamishwa kiholela, na wakati mwingine kupelekwa maeneo ya pembezoni mwa nchi.21
Zaidi ya hayo, maamuzi ya vyombo vya kikanda vya utoaji wa haki, (ambapo kimsingi vyombo hivi vinapaswa kuwa tegemeo la mwisho na kimbilio la utoaji haki), hayaeshimiwi wala kutekelezwa. Mwaka 2011, Mahakama Kuu ya nchini Venezuela ilibatilisha maamuzi ya Mahakama ya Kikanda ya Ukanda wa Amerika yaliyoelekeza kuondolewa kwa zuio/katazo la kutoshiriki uchaguzi kwa mwanasiasa wa upinzani nchini humo Bw. Leopoldo López, na kudai kuwa uamuzi huo hautekelezeki, kwani unakiuka katiba ya nchi, na pia unaingilia uhuru wa jamhuri ya Venezuela.22 Uturuki imepuuzia amri ya Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu, iliyoamuru kuachiliwa huru kwa mhisani na kiongozi wa kisiasa Bw. Osman Kavala, pamoja na mwanasiasa wa upinzani Bw. Selahattin Demirtaş. Kwa upande wa Tanzania, mwaka 2019 serikali iliamua kuwaondolea raia wake haki ya kufungua kesi moja kwa moja katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu. Katika mahakama hiyo, Tanzania ilikuwa ni nchi kinara kwa kesi na hukumu nyingi zilizokwisha tolewa dhidi yake.23
Kukosekana kwa uhuru wa mahakama hasa katika mifumo, kunaacha nafasi ndogo kwa wakosoaji na wapingaji wa serikali kutafuta na kupata msaada wa kisheria pindi wanapokabiliwa na vifungo vya kisiasa ama kifo cha uraia. Japo uvumilivu wa baadhi ya majaji wenye fikra na misimamo huru, kunaonekana kama chanzo cha matumaini, kiuhalisia bado wana kinga ndogo sana dhidi ya serikali, na hivyo inawapelekea kufanya kazi katika hali hatarishi.
- 1Inter-American Commission on Human Rights, “Nicaragua: Concentration of power and the undermining of the Rule of Law,” October 25, 2021, https://www.oas.org/en/iachr/reports/pdfs/2021_nicaragua-en.pdf.
- 2Inter-American Commission on Human Rights, “Persons Deprived of Liberty in Nicaragua,” October 5, 2020, http://www.oas.org/en/iachr/reports/pdfs/Nicaragua-PPL-en.pdf.
- 3UN Human Rights Council, Report of the independent international fact-finding mission on the Bolivarian Republic of Venezuela, A/HRC/48/69 (December 28, 2021).
- 4UN Human Rights Council, Report of the independent international fact-finding mission on the Bolivarian Republic of Venezuela, A/HRC/45/33 (September 25, 2020).
- 5Gareth H. Jenkins, “From Politicization to Monopolization? The AKP’s New Judicial Reforms,” Turkey Analyst 4, no. 3 (February 7, 2011), https://www.turkeyanalyst.org/publications/turkey-analyst-articles/item….
- 6Freedom House, “Turkey,” in Freedom in the World 2023, https://freedomhouse.org/country/turkey/freedom-world/2023.
- 7Nóemi Lévy-Aksu, “Turkish Constitutional Court rules that the convictions of Academics for Peace violate their rights,” London School of Economics and Political Science Department of Gender Studies, January 2020, https://www.lse.ac.uk/gender/news/2020/Turkish-Constitutional-Court-rul….
- 8Amnesty International, “Tunisia: President’s moves to shut down High Judicial Council pose grave threat to human rights,” February 8, 2022, https://www.amnesty.org/en/latest/news/2022/02/tunisia-presidents-moves….
- 9Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights, “Tunisia: Presidential decrees undermine judicial independence and access to justice, says UN expert,” July 15, 2022, https://www.ohchr.org/en/press-releases/2022/07/tunisia-presidential-de….
- 10Human Rights Watch, “Tunisia: President Intensifies Attacks on Judicial Independence,” February 27, 2023, https://www.hrw.org/news/2023/02/27/tunisia-president-intensifies-attac….
- 11Interview with a former Tunisian political prisoner who requested anonymity, July 2023.
- 12Interview with a representative from the Center for Defenders and Justice, July 2023.
- 13Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights, “Thailand: UN rights expert concerned by the continued use of lèse-majesté prosecutions,” February 6, 2017, https://www.ohchr.org/en/press-releases/2017/02/thailand-un-rights-expe…; “Compare civilian and military courts when dealing with lese majeste cases,” Prachatai, December 3, 2014, https://prachataienglish.com/node/4554.
- 14İnsan Hakları Ortak Platformu, “21 July 2016-20 March 2018 State of Emergency in Turkey: Updated Situation Report,” April 17, 2018, https://www.ihop.org.tr/en/wp-content/uploads/2018/04/SoE_17042018.pdf.
- 15Turkey Tribunal, “Mass Dismissals of Judges and Prosecutors in Turkey of Post-Coup Period,” April 21, 2022, https://turkeytribunal.org/actuality/mass-dismissals-of-judges-and-pros….
- 16“Tunisia Cuffs Two Former Judges,” Voice of America, February 13, 2023, https://www.voaafrica.com/a/tunisia-cuffs-two-former-judges/6960771.html.
- 17Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights, “Tunisia: Judges’ right to association and protest must be respected, say UN experts,” September 14, 2022, https://www.ohchr.org/en/press-releases/2022/09/tunisia-judges-right-as….
- 18See, for example, interviews with Christopher Hernandez-Roy, Senior Fellow and Deputy Director, Americas Program, Center for Strategic and International Studies, August 2023; Tamara Taraciuk Broner, Rule of Law Program Director for Inter-American Dialogue, August 2023; and Franz von Bergen, Venezuelan journalist, June 2023.
- 19Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights, “Venezuela: UN expert condemns further sentence against Judge Afiuni, says clearly act of reprisal,” March 26, 2019, https://www.ohchr.org/en/news/2019/03/venezuela-un-expert-condemns-furt….
- 20“Clash between Constitutional and appeals courts raises concerns over rule of law in Turkey,” Associated Press, November 9, 2023, https://apnews.com/article/turkey-high-courts-clash-imprisoned-lawmaker…; Media and Law Studies Association (MLSA), “Constitutional crisis - Can Atalay Controversy in the Judiciary,” November 9, 2023, https://www.mlsaturkey.com/en/constitutional-crisis-can-atalay-controve….
- 21UN Human Rights Council, Detailed findings of the independent international factfinding mission on the Bolivarian Republic of Venezuela, A/HRC/48/CRP.5 (September 16, 2021); interview with a Tanzanian civil society actor who requested anonymity, July 2023.
- 22Human Rights Watch, “Venezuela: Implement Inter-American Court Ruling,” September 20, 2011, https://www.hrw.org/news/2011/09/20/venezuela-implement-inter-american-….
- 23Amnesty International, “Tanzania: Withdrawal of individual rights to African Court will deepen repression,” December 2, 2019, https://www.amnesty.org/en/latest/press-release/2019/12/tanzania-withdr….
Nini Kifanyike
Vifungo vya kisiasa na mbinu za kifo cha uraia ni nyenzo muhimu kwa viongozi wa tawala za kiimla na zisizokuwa za ki-demokrasia, ambapo huzitumia katika lengo na jitihada za kuwanyamazisha na kuwaondoa kwenye jamii wakosoaji wenye misimamo mikali. Vile vile, utumiaji wa mbinu za hila za kifo cha uraia dhidi ya wapinzani wa serikali, husaidia mamlaka kukwepa uchunguzi na kufuatiliwa na jumuiya za kimataifa, ambao mara nyingi hutokana na vifungo vya kisiasa. Katika kila nchi kwenye nchi zote sita zilizofanyiwa utafiti, tumeanisha kuwa vifungo vya kisiasa na mbinu za kifo cha uraia hutumika kuwaadhibu wapinzani wa serikali wanaofanya jitihada na kazi ya kutetea demokrasia na haki msingi za binadamu. Pia tuliweza kutambua kuwa majaribio haya ya kuwaondoa wakosoaji na wapingaji wa serikali katika jamii, kuliambatana na nyakati za uporomokaji mkubwa wa demokrasia katika nchi husika.
Photo: ZUMA Press, Inc./Alamy Stock Photo
Licha ya madhila, mateso na usumbufu ambao watetezi wa haki za binadamu, wanaharakati wa demokrasia, waandishi wa habari, wanasiasa wa upinzani, waandamanaji na watu wa kawaida wanaopitia, au wako katika hatari ya kupitia hasa katika nchi zenye utawala wa kiimla; uwepo wa baadhi ya watu wachache mashujaa wanaofanya kazi ya kufichua na kupambana na udhalili na udhalimu wa tawala za kiimla na kimabavu, unatoa sababu ya matumaini ya kupata mabadiliko ya kidemokrasia katika nchi hizo. Hata katika hali hatarishi, bado asasi za kiraia zimeendelea kuandaa na kuchapisha ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na watawala, huku pia zikiendelea kutoa msaada kwa wahanga wa ukiukwaji wa haki za binadamu. Mawakili wa utetezi wameendelea kuwatetea wateja wao ama wafungwa ambao wamesota gerezani muda mrefu, wamefungwa kwa madai yasiyo na msingi, au wamezuiwa kusafiri, na ndugu ambao wamejitokeza kupinga vifungo holela na visivyo haki vya wapendwa wao, wanaotafuta suluhu na kupigania ndugu zao kuachiliwa huru. Na katika kufanya hivyo, wanaungana na wengine ambao wanapitia changamoto kama zao. Katika upande wa mahakama, bado wapo majaji na mahakimu wachache wasio na upendeleo ambao bado wanafanya kazi kwa kuzingatia hatua stahiki na taratibu za kisheria na kukataa kutoa vifungo au hukumu zenye sura ya kisiasa. Hata hivyo hatari hii ambayo wameamua kuibeba inaonesha na kuthibitisha umuhimu wa kuzuia mashambulizi juu ya uhuru wa mahakama.
Jitihada hizi zote zinazofanyika, zinatumika kuwakumbusha watetezi wa demokrasia na utawala bora kuwa, mapambano ya kupata uhuru hasa wa mahakama katika mazingira magumu, sio kitu kinachopotea bure. Moja ya hatua muhimu ambayo jumuiya za kimatifa na serikali za kidemokrasia zinapaswa kuchukua ili kuunga mkono utetezi juu ya uhuru wa mahakama katika nchi husika ni kushinikiza kuachiwa bila masharti yeyote kwa wafungwa wa kisiasa.
Hata hivyo, ni vyema kutambua kuwa changamoto na matatizo ambayo wafungwa wa kisiasa na familia zao wanakabiliana nayo hayakomi tu baada ya kuachiliwa kwao. Hivyo basi, ni muhimu kuandaa rasilimali na kuwapatia msaada wafungwa wa kisiasa, kama vile msaada wa kisaikolojia na matibabu. Wakati huo huo, kutambua na kuziangazia namna na mbinu mbalimbali zinapopelekea kifo cha uraia ni muhimu katika kukabiliana na utawala wa kimabavu na kiimla, na hatimaye kusaidia kuzuia wimbi kubwa la ukiukwaji wa sheria na ukandamizaji kwa nyakati za usoni.
--
Sign up to receive the Freedom House weekly newsletter.